Jamii inawezaje kuleta mabadiliko katika elimu?

555112_625260264156606_342220663_nElimu ni mchakato rasmi unaozalisha watu wenye maarifa,ubunifu na uwezo wa kufikiri,kujitambua pamoja na ujuzi wa aina mbalimbali wanaotumia kuunda vitu anuai ili kujiletea maendeleo. Karibu jamii zote kwa sasa zinaamini kuwa elimu bora ni daraja la maendeleo kwa jamii husika.

Bila elimu bora ni ngumu mno kupata maendeleo ya haraka katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kwasababu elimu inahusu jamii, kwa manufaa ya jamii na kwa wanajamii wote ni vyema jamii ikawa mstari wa mbele katika kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa watoto wao ili waje kuwa watu muhimu katika jamii.

Jamii ina jumuisha wazazi ambao wanawajibu wa kuzaa watoto na inatolewa shule ili wapate maarifa takikana na stadi nyingine muhimu katika maisha.  Isitoshe, mzazi anapaswa kumpatia mtoto wake mahitaji yote muhimu ya shule ili pamoja na maadili na ushauri chanya ili mtoto akue katika maadili bora yanayokubalika katika jamii.

Mtoto asiye na maadili na mwenendo bora ni msiba kwa mzazi, mwalimu na jamii kwa ujumla. Ni sawa na gari linalosafiri usiku bila taa.

Jamii pia inawajibu wa kufuatilia na kufahamu sera za elimu zinazotolewa na serikali ili wajue zinasema nini na kuzijadili kulingana na mahitaji yao. Bila kufahamu sera jamii itakosa ujasiri wa kuhoji mipango mbalimbali inayofanyika katika jamii yao na hasa mipango mibaya isiyokidhi mahitaji au matarajio yao. Jamii itabaki gizani siku zote.

Na wanaoumia zaidi ni jamii ya watu masikini ambao wanahitaji sana elimu kwa watoto wao, maana huo ndio ukombozi wao. Jamii ni muhimu kufuatilia mchakato mzima wa kujifunza kwa watoto pia. Suala hili kwa wengine linaonekana kama ni kazi ya mwalimu tu.La hash!

Mzazi lazima ajue mtoto anafanya nini shuleni, ana uwezo gani, ana matatizo gani ili ayatatue au kushirikiana na mwalimu kuyatatua.

Mzazi anapokuwa mbali na mwalimu ni vigumu mno kwa mtoto kufanikisha lengo la kuwa shule. Kuwaachia walimu tu sio sahihi na kuwakatisha tama walimu. Tuwakunje samaki nyumbani wangali wabichi, maana wakisha kauka walimu hawataweza kuwakunja.

Jamii ishiriki kikamilifu katika kuibua mijadala mbalimbali ihusuyo maboresho ya sekta ya elimu. Pale pale ulipo unaweza kuleta mabadiliko kwa kushiriki katika vikao vya serikali, kamati za vijijini na hata vikao vya serikali za mitaa vinavyojadili maendeleo ya eneo husika.

Katika mikutano na vikao hivyo, ndimo huzaliwa mambo mengi kama mipango endelevu ya kuboresha utoaji elimu. Kujadili mapato na matumizi ya shule, mapungufu ya pesa za uendeshaji na hata kushiriki kuhoji matumizi mabaya ya pesa.

Jmaii inapogeuka kuwa watekelezaji tu wa kile kilichaamriwa toka juu bila kujua athari zake ni jamba ambalo hushusha maendeleo ya jamii husika. Maana wanajamii wanaoizunguka shule fulani ndio wanajua kwa kina matatizo na mafanikio ya shule yao.Na ndio inawahusu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.

Hivyo, kushindwa kuyajadili kwa kina matatizo yanayoikabili shule yenu kwa uwazi na umakini ni kuficha tatizo. Waziri hawezi kuyajua matatizo ya shule ya msingi Chabutwa au sekondari kama hajafika au kupelekewa taarifa. Yeye muda mwingi anategemea taarifa toka kwa watendaji wake wa chini. Na baadhi ya watendaji wake hao sio makini na wanaajenda zao na hivyo siku zote wanafanya kazi kwa mazoea tu bila ubunifu wala kuwa na uchungu na shule au jamii.

Hivyo, basi kuwa na jamii yenye uchungu na maendeleo ya watoto wanaosoma katika shule hizo, hasara huwa ni kwa jamii ya mahali hapo husika sio watendaji wa serikali. Maana watendaji wengi ni watu wa kuja, na watoto wao wengi wanasoma shule bora zenye mazingira mazuri mijini.

Jamii lazima ielewe kuwa shule kukosa mwalimu sio hasara ya waziri, wala Afisa elimu au katibu mtendaji wa kijiji. Hasara ni kwa wanajamii hasa wazazi wa watoto.

Hata kufeli kwa watoto kuliko tokea mwaka 2007 na 2012, Waziri hajapata hasara yeyote ila wazazi wenye watoto na watoto wenyewe ndio wenye hasara kubwa.

Yapo matatizo ya mimba za utotoni ambazo zinaangamiza watoto wa kike. Na baadhi ya maeneo wahusika wanafumbiwa macho na jamii husika. Haya yanapaswa kujadiliwa kiuwazi kabisa na kupatiwa suluhu kwa kuwajibisha wahusika.

Zaidi, watu wenye ulemavu wengi wao wanafichwa ndani na jamii inangalia tu bila kuchukua hatua. Wanaendelea kubaki nyuma kielimu na kimaendeleo.Jamii inafurahia hilo?

Matatizo ni yetu, tuyajadili kwa pamoja na kuyapatia suluhisho. Ukimya hauzai! Kuficha matatizo ni kukuza tatizo, woga na umbumbumbu hauna nafasi katika ulimwengu wa haki na maendeleo. Tuhoji! tujadili! tutoe mapendekezo ya utatuzi na tuongeze utelezaji.

Je jamii inapata faida gani kuona watoto wanafeli mitihani na kubaki nyumbani tu? Wazazi waliowapeleka watoto shule walitarajia hayo? Hadi lini tukae kimya kwa maswala yanayotuhusu? Na faida za kukaa kimya ni zipi?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.