Vyanzo vya Maarifa Vinajulikana?

Moja ,Elimu ni chanzo cha kwanza cha maarifa kwa binadamu. Elimu ambayo ni mchakato rasmi au sio rasmi wa kujifunza ndio maarifa ya kila namna hupatikana. Mwalimu kama muwezeshaji wa kwanza, humjengea mtu ari ya kutaka kujifunza kila siku na kumpatia mbinu za kujifunza.

Katika mchakato huo wa kujifunza ndipo mwalimu kama huweza pia kuhamisha maarifa kwenda kwa wanafunzi na kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kujifunza ili awe mpenda kujifunza siku zote. Maana elimu haina mwisho. Bila kuwa na walimu wenye sifa za ualimu, maarifa ambayo ndio elimu yenyewe inakuwa vigumu kupatikana au yanapatikana nusunusu.

Pili,Vitabu ni chanzo kingine cha maarifa. Kila aina maarifa takikana yamo ndani ya vitabu. Yameandikwa tangu enzi za mababu zetu. Mathalani kwa waumini wa dini Biblia na Quran ni vitabu vya siku nyingi vyenye maarifa ya hali ya juu ambayo kamwe hayapitwi na wakati.

Tatu, Maandiko ya wanafalsafa. Wako wana falsafa kama akina Socrate, Plato, Jean Jaques, Rossauau, Paul Freire wameandika kanuni mbalimbali zenye maarifa tele ambazo hadi leo zinamsaidia binadamu kufanya maendeleo makubwa. Wapo pia akina Issack Newton ambao sidhani kama watakuja kusahaulika. Maandishi na vitabu vya hawa ni chanzo cha maarifa mengi kwa binadamu.

Pamoja na kuwa ukweli huu ni dhahri, je watanzania wangapi husoma vitabu? Maktaba nyingi zimefurika vitabu vyenye kila aina ya maarifa, lakini watu wengi hawana utamaduni wa kusoma vitabu.

Pata Habri kwa Urahisi
Pata Habri kwa Urahisi

Hata wasoni tunaotegemea huko vyuoni ni wachache wenye utamaduni wa kusoma vitabu. Wengi wanapenda njia za mkato.Je tutapaje maarifa kama hatuna utamaduni wa kusoma vitabu? Mwanafalsafa wa kimarekani John Khan aliwahi kusema ni bora ukose chakula kipindi Fulani lakini upate kitabu.

Ukweli huu aliutambua sana Mwalimu Nyerere ndio maana alikuwa msomaji mahiri wa vitabu. Pia alijua utakufa akaamua kuacha wingi wa maarifa kwa kuyaandika kwenye vitabu. Je hata vitabu vya Baba wa taifa tunavisoma? Au vipo kwenye makabati na mashelfu tu?

Nne, Vyombo vya habari.Inasemekana vyombo vya habari ni muhimili wanne wa dola/nchi yeyote. Kama hili ni kweli, basi umuhimu wa magazeti, Redio, Luninga, Intaneti na majarida ni mkubwa mno.

Vyombo vya habari ni chanzo cha maarifa. Kwa hiyo,tunapata maarifa mbalimbali, tunapata habari za matukio ya kila aina yanayotokea kila siku, tunapata taarifa kwa muda unaotakiwa na pia burudani. Tunapata mafunzo na maonyo yanayosaidia kumfanya binadamu makini ajiboreshe kila siku.

Taifa bila vyombo vya habari ni kama gari bila taa linasafiri usiku gizani. Tujiulize tena, Ni watanzania wangapi husoma magazeti? Ni watanzania wangapi husikiliza radio na kuangalia taarifa za habari na vipindi vingine kwenye luninga?

Ni kweli bado kuna jamii ambazo upatikanaji wa habari kwao ni tatizo kutokana na mazingira au umasikini.Lakini kwa watanzania wengi vyombo hivi vya habari vimesambaa hadi vijijini. Kwa sasa ni vigumu kukuta kijiji kizima hakuna Radio. Jamii kubwa inapata habari kupitia vyombo mbalimbali.

Pengine tatizo ni utashi wa wanajamii wenyewe kutafuta habari. Wapo watu wenyewe kutafuta habari.Wapo watu wasiopenda kabisa kusoma hata gazeti au kitabu. Tena hawa ni wengi hapa kwetu Tanzania. Mtu mwenye utamaduni wa kujisomea siku zote ana ari ya kutafuta habari.

Na huwa tofauti sana na mtu asiyejishugulisha kutafuta maarifa wala habari.Hata kama ni msomi wa namna gani ,kama ataridhika na usomi wake kisha akabweteka ,kamwe atabaki msomi wa cheti tu. Maana maarifa kila siku yanazaliwa mapya na hakuna mtu yeyote duniani anayejua yote.

Msomi wa shahada ya uzamivu (PhD) kwenye fani ya mawasiliano aliyeipata miaka ya 1980, nadhani hawezi kuwa mahiri wa teknolojia za sasa za mawasiliano japo ni msomi. Maana mambo mengi wakati anasoma hayakuwepo. Hivyo, bila kujishughulisha atabaki mbumbumbu kwenye eneo hilohilo alilopatia PhD, hadi asome tena ili ajue mapya.

Bila juhudi binafsi ni vigumu kupata maarifa au habari. Mfano unaweza kuwa na luninga lakini huiwashi, unaweza pia kuwa na gazeti lakini hulisomi. Hapa hakuna tofauti na yule ambae hana. Maana wanafalsafa husema kitabu usichokisoma ni sawa na hakipo!

Ni muhimu kujua kuwa binadamu hajegwi kama nyumba. Nyumba ndio hujengwa kuanzia msingi hadi kupaka rangi. Lakini binadamu hujijenga mwenyewe kwa juhudi binafsi za kujisomea na kutafuta habari. Hakuna mtu anayeweza kumjenga mwenzie muda wote. Hata walimu kazi zao kujifunza na kuonesha njia ili mwanafunzi ajenge utamaduni wakujisomea muda wote hadi uzeeni.

Hii inashabihi usemi usemao elimu ni bahari haina mwisho.Wingi wa maarifa ni utajiri wa leo na kesho. Bila maarifa huwezi kupata maendeleo.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.