Hali halisi ya Ualimu : Jukumu letu sote Kutimiza Wajibu

Ualimu ni nyanja muhimu katika Taifa lolote kwa mustakabali wa ubora wa Elimu kwa wananchi, maendeleo katika jamii na ukuaji wa uchumi. Wataalamu wengi  nchini katika sekta mbalimbali wanatokana na mwalimu. Mwalimu ndie aliyewajengea msingi mpaka kufikia hapo walipo.dsc002071.jpg

Lakini tukiangalia hali halisi ya walimu Tanzania ni duni kiasi cha kukatisha tama. Hali waliyonayo walimu wa Tanzania inafanya kazi ya ualimu kuwa ngumu na pia inawafanya watu wazidi kutoipenda.

Hali halisi inajionesha katika mazingira ya kufundishia, ukosefu wa vifaa vya kufundishia na idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa lisilo na samani, mshahara mdogo wa walimu ambao hawapati kwa wakati, ukosefu wa mafunzo kazini ya kumwendeleza mwalimu na usambazaji duni wa walimu ambao hupendelea kufundisha shule za mijini kuliko vijijini.

Matumaini, ujasiri na kujituma kwa walimu leo hii kumetoweka hali ambayo inajionesha katika ufundishaji madarasani. Mwalimu hana muda wa kutumia mbinu wala njia yeyote ile ya kumfanya mwananfunzi ajifunze.

Kazi imebakia ni kumwelekeza mwanafunzi namna ya kujibu maswali ili afaulu mitihani bila kujali anaelewa anachojifunza au laa. Hali inayopelekea kupata maajabu ya watoto kufika shule za sekondari bila kujua kusoma na kuandika ipasavyo.

Hali hii mpaka lini, walimu tubadilike na tuone suala la kuwalea watoto na kuwapatia maarifa katika kujifunza ni jukumu letu kwani tukumbuke hata dini zetu zinatueleza kuwa tutakuja kuulizwa kwa kile tulichokifanya duniani basi iwe ni kwetu kujituma na kufanya kwa Baraka zetu na maslahi yaje kwa mustakabali mwingine. Tuwasaidie wanafunzi wetu kama wenetu.

Nasi wanafunzi tuwe chachu ya amani, furaha na faraja kwa walimu wetu ili wajione wanacho wanachojivunia licha ya hali halisi ilivyo kwani kwa kufanya hivyo ni moja ya kuibadilisha hali halisi na kupigania mapinduzi ya kweli ya haki zetu.

Wanajamii tuna kila sababu kuwa mstari wa mbele katika kuangalia elimu wanayopatiwa wanetu na tujiulize maswali kama kweli ndo tunachokihitaji kwa watoto wetu tunapowapeleka shule? Kama sicho basi itupelekee tupaze sauti zetu juu ya hali ya elimu nchini mwetu, tutoe mapendekezo na tushiriki katika kusaidia uboreshwaji wa elimu kwa ajili ya vizazi vyetu na vya wanetu.

Na kama wewe ni miongoni mwa watunga sera au una mamlaka ambayo yanaweza kupelekea kubadili hali hii ya elimu nchini mwetu basi tafakari na sikiliza vilio vya walimu, wanafunzi na wanajamii  iwe ni jukumu lako kuchukua hatua na kubadili hali halisi ili kuleta ufanisi na maendeleo nchini mwetu.

……..kila kitu kinawezekana sote ni chachu ya mabadiliko kufikia maendeleo endelevu ya kweli katika elimu.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Hali halisi ya Ualimu : Jukumu letu sote Kutimiza Wajibu

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.