Wadau mbalimbali tuna amini kwamba elimu bora inapaswa kuelekezwa kwenye stadi na ujuzi wa wanafunzi. Ili kufanikisha matokeo hayo muhimu, tunahitaji vitendea kazi-madarasa, walimu, vitabu vya kiada, maktaba, maabara na mazingira safi na salama.
Ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, tunahitaji kujiuliza wenyewe;
Ni nini kinafanyika darasani? Walimu na wanafunzi wanafanya nini kufanikisha kujifunza? Ni jinsi gani wanatumia vitabu vya kiada, maktaba na maabara? Je, kila kitu kimepangiliwa kwa ajili ya watoto wetu kujifunza stadi wanazohitaji baadaye?
Wakati muafaka wa kuhamia kwenye elimu bora ni huu.
Tengeneza mitaala inayokubalika
Program ya elimu ni lazima ielekezwe kuendeleza stadi za watoto wanaohitaji kufanikiwa katika jamii.
Boresha mafunzo ya walimu
Walimu wanapaswa kulielewa vyema somo wanalofundisha. Wanapaswa kuwa msaada muhimu kuwapa hamasa wanafunzi katika somo na kuyafurahia masomo.
Upimaji halisi
Mtihani mmoja usiamue hatma ya baadaye ya watoto. Tunahitaji njia mbalimbali za kupima maarifa na stadi za watoto.