MWONGOZO WA MBINU ZA KUFUNDISHIA SHULE ZA AWALI: SEHEMU YA PILI

Zana za Kufundishia

Kwa kuzingatia ufundishaji na hali halisi ya watoto wadogo, mwalimu anashauriwa kutumia ubunifu wake ili kupata vifaa vingi iwezekanavyo kwa kila aina ya vitendo. Mtoto anapaswa kuandaliwa na kutumia vifaa vinavyofaa kufundishia kila mada, kwa sababu hiyo mwalimu anashauriwa kutumia maarifa, stadi na uzoefu katika kuchagua mbinu na njia za kutumia kulingana na mazingira ya kijamii kutoka shule moja hadi nyingine.

Zana za Kufundishia na Kujifunzia
Zana za Kufundishia na Kujifunzia

Njia za Kufundishia na Kujifunzia

Mwalimu anashauriwa kuwahusisha watoto katika somo kwa njia za maelekezo, maswali mafupi pamoja na vitendo. Watoto watumie milango ya fahamu, kugusa, kuona, kusikia, kunusa na kuonja.

Hivyo kuna ulazima mwalimu kutumia vitu halisi, vifani, picha na vielelezo vingine katika kuwawezesha watoto kuelewa mada iliyo kusudiwa.

Tathmini ya Maendeleo na Uwezo wa Watoto

Kwa kawaida watoto wa darasa la awali hawapewi mitihani kama wapewavyo shule za msingi. Kutakuwa na upimaji wa maendeleo ya watoto kwa kuangalia uwezo wake. Kazi hii inafanywa kwa kuangalia kumbukumbu za maendeleo ya mtoto tangu alipoanza kuhudhuria shule ya awali hadi anapomaliza na kuandikishwa katika darasa la kwanza.

Ni muhimu mwalimu awe na utaratibu wa kuweka kumbukumbu zao.

Ubora wa Mwalimu

Ieleweke kuwa mwalimu ni nyenzo muhimu na kuu katika harakati za kufundisha na kujifunza. Ubora wa mwalimu kwa kiasi kikubwa unahusishwa na uwezo wake wa kumudu somo au mada anayofundisha. Aidha ufundishaji bora ni ule unaofanikisha na kuhusisha uchaguzi wa njia na mbinu sahihi za ufundishaji pamoja na vitendo vingi kufanywa na mwanafunzi badala ya mwalimu.

Maswali

 1. Taja madhumuni makuu manne (4) ya Elimu ya Awali.
 2. Taja sifa kuu nne (4) za Mwalimu wa Elimu ya Awali.
 3. Eleza kwa kifupi, Ubora wa Mwalimu ni upi?
 4. Taja mbinu mbalimbali zinazofaa kufundishia watoto wa shule ya awali.
 5. Taja vigezo vine (4) vinavyofaa kutumiwa na mwalimu wa Elimu ya Awali katika kuchagua mbinu na njia za kufundishia darasa lake.
 6. Nini maana ya zana za kufundishia na kujifunzia?
 7. Taja aina tatu (3) za zana za kufundishia na kujifunzia.
 8. Taja vitendo sita (6) vya masomo vinavyofundishwa katika shule za awali.
 9. Fafanua istilahi zifuatazo;
  1. Vitendo vya masomo
  2. Vitendo vya kujifunza
 10. Mazingira mazuri yanayovutia yanamsaidia mtoto kujisikia vizuri na kufurahia kuwepo shuleni. Mtot anapaswa awe huru na kuchunguza, kudadisi, kuuliza maswali na kujifunza. Ili mtoto apate uhuru huo mwalimu anapaswa kufanya mambo gani? Jadili.
 11. Kazi mradi (project) ni njia ya kufundishia ambayo huwafanya watoto wa elimu ya awali kujifunza kwa kushirikiana. Fafanua na toa mifano.
 12. Hakuna njia moja tu inayokidhi haja zote za kufundisha. Mwalimu fanisi ni Yule anayeweza kutumia njia zaidi ya moja wakati anapofundisha mada au somo. Fafanua.
 13. Eleza jinsi utakavyoweza kumsaidia;
  1. Mwanafunzi mwenye tabia ya utoro wa shule.
  2. Mwanafunzi anayeshindwa kujifunza.
  3. Mwanafunzi mwenye matatizo ya kuumwa mara kwa mara.
 14. Jadili, ni lini hasa unaweza kutambua kuwa mwanafunzi amepata maarifa, stadi na mwelekeo?
 15. Mtoto anajifunza kutokana na maarifa ya awali aliyonayo na jinsi anavyojihusisha na mazingira. Fafanua kauli hiyo.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “MWONGOZO WA MBINU ZA KUFUNDISHIA SHULE ZA AWALI: SEHEMU YA PILI

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.