SIASA ZA UCHAGUZI 2010-2015

Imeandikwa na Nyanda Josiah Shuli
Imeandikwa na Nyanda Josiah Shuli

Naelekea kuchukia siasa zinazofanywa nchini kwetu. Kwa bahati mbaya sana zimekuwa ni siasa za uchaguzi tu. Aliyeko madarakani kazi yake ni kung’ang’ana asinyang’aywe tonge…aliye nje kazi yake ni kutaka kumwangusha aliyeko madarakani…siku moja yeye ndiye aaminiwe zaidi. Mitazamo yote hii miwili inatuletea siasa dhaifu sana. Leo hii wanasiasa wa vyama tofauti hawajui… na hawataki kufanya kazi kwa pamoja.

Hata katiba ambalo ni andiko la watanzania wote linataka kutekwa na wanasiasa…naelekea kuamini kwamba hata vyama mbadala wangepewa nafasi kuandika katiba mpya….ili tuichukue na kuipitisha bila maswali, nao wangeandika mambo yao tu. Wangejikita kwenye mambo yanayohusu taratibu za uchaguzi, muundo wa serikali na mambo ya tawala. Kimsingi hayo ndiyo baadhi ya mambo yaliyowafanya wadai katiba mpya.
Kila mwanasiasa angetambua kwambua kwamba Tanzania ni kubwa kuliko chama chochote kile, ni kubwa kuliko mtu yeyote yule. Sote tutapita na kwenda zetu…Tanzania itabaki. Ni Mungu mwenyewe ndiye ataendelea kuionabTanzania kila siku wakati ‘wachonga ngenga’ walishapita na wakapotea, watukanaji bungeni walishapita na kupotea, wadini walishapita na kupotea, nk…ila kwa bahati mbaya sana watakuwa wametuachia makovu ya kufumu-Mungu atuepushe na hili.
Bila wanasiasa wa itikadi tofauti kujua lini wapige siasa za uchaguzi na lini washirikiane kuleta maendeleo kwa watanzania na Tanzania tutakuwa kila siku tuko kwenye mashindano kama vile ya riadha. Fikiria mkimbiaji hodari Usian Bolt angekuwa anashindana kila siku, angeshachoka, angeshafulia, angeweza kushindwa na hata mtu dhaifu. Kwa nini wanasiasa wasiwe na mikakati ya kuhifadhi sehemu ya nguvu zao mpaka wakati muafaka ufike? Istoshe, kwa wale watakaofanya siasa za maendeleo watakuwa wamejiwekea mazingira mazuri baadaye.
Kila chama kinafanya siasa za uchaguzi toka 2010 mpaka 2015; mbaya zaidi siasa hizi zimeingia hadi ndani ya vyama hivi na kutengeneza makundi makubwa ambayo hayashirikiani kwa lolote. Ni mahasimu wa kisiasa. Hata uchaguzi wa 2015 ukiisha, zitaanza siasa za uchaguzi wa 2020.
Naanza kusadiki kwamba demokrasia ya kimagharibi imekuja mapema sana nchini kwetu. Wanasiasa, ambao ndio watawala wa sasa au watawala wa baadaye wameweka akili zao kwenye chaguzi, badala ya maendeleo. Mifano ipo mingi sana ya nchi ambazo tulilingana nazo kimaendeleo wakati tunapata uhuru-lakini wao wako mbali sana sasa. Kwa nini? Wao wanafanya siasa za uchaguzi-baadaye wanaelekea kwenye siasa za maendeleo mara chaguzi zinapoisha.
Kwa siasa zetu…hata tukibadili vyama katika utawala wa nchi tutaendelea kuvuna mabua. Wakenya wameshajua namna ya kushirikiana kama vyama. Lini washirikiane na lini waachane. Sisi kila siku tunaishia kuona kila linalofanywa na chama tofauti na tulichopo ni baya, halifai. Nimekosa imani na siasa za Tanzania. Nikiwa mtaalam wa mawasiliano nina mengi ya kuwashauri wanasiasa, ama vyama vya siasa-hasa namna ya kujenga mguso wa kudumu mioyoni mwa wananchi.
Mwl Nyerere alifanikiwa sana katika hili-bila kutumia makada waongo waongo, bila kutumia helkopta na bila kuwa na mitandao ya kushughulikia kambi tofauti au vyama tofauti. Kuna mbinu za kufanya hivyo-na hazina madhara wala kuhitaji bajeti kubwa. Niko tayari kuwashauri wenye nia ya kubadilika bila malipo.
Inakera sana kuona Bunge-tena la bajeti likiishia kwenye malumbano ya kiitikadi tu-huku likidonoadonoa bajeti kwa mbali-na propaganda zikichukua sehemu kubwa. Vyama vikuu CCM na CDM wamejielekeza huko. Nani atajadili bajeti? Labda TLP, UDP, NCCR na CUF. Je, peke yao wataweza? Istoshe nao wako kwenye ugonjwa ule ule wa siasa za uchaguzi…wa taifa au wa ndani ya vyama.
Poor Tanzania!

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.