Wananchi tusiridhike na elimu isiyokuwa na tija

Nguvu muhimu ya kuchochea maendeleo katika jamii yeyote ni elimu bora. Elimu ambayo itawajaza wananchi maarifa tele, uwezo wa kufikiri, ujuzi wa mbinu mbalimbali za kutatua matatizo, ubunifu, ujasiri wa kuhoji, kudadisi, kujitambua na moyo wa uvumbuzi na fikra mpya zenye kutafsiri na kuzibadili changamoto kuwa fursa.

603887_519562718086200_1070368810_nElimu ya namna hii ndiyo inajenga daraja la maendeleo. Maana jamii kubwa ya watu itakuwa na uwezo wa kuzalisha na kushiriki moja kwa moja katika kujenga taifa lao.

Jitihada zetu za kujiletea maendeleo hazitaweza kufanikiwa iwapo elimu ya namna hii haipo katika jamii.

Na wananchi wakiwa wamelala bila kuhoji elimu yetu ya sasa inayotengeneza vyeti bandia na wasomi bandia hali itakuwa ngumu mno.

Wananchi kwa sasa tumeridhika na hali ya maisha. Hatufikirii vya kutosha  namna ya kuiboresha elimu yetu. Tumeridhika na vipimo dhaifu vya nini maana ya elimu na mazao yake katika jamii.  Lakini ukweli unasaliti kwa kuwa na wasomi wengi wasio na tija katika jamii.

Pamoja na kuelekeza jitihada zetu kwenye vitendea kazi kama vile majengo, madawati, sare za shule, vitabu, chaki, pesa na hata chakula na usafiri, yatupasa vilevile kuelekeza nguvu kwenye elimu; yaani nini mtoto anapata awapo shule. Hii ni kama vile mtoto ana maarifa gani, amefahamu nini baada ya kusoma, anaweza kufanya nini, anajiamini, anaweza kuthubutu, anaweza kuwasiliana vizuri, anajitambua, ni mbunifu, ni mvumbuzi, anajitihada za kufanyakazi, ni mjasiri na mwadilifu.

Hivyo, watanzania tuwe makini tutumie muda mwingi kukaa na watoto wetu na tuwapime ili kuhakikisha wanapata elimu kwa kutathimini viashiria vya elimu vilivyoainishwa. Na ndipo tutabaini ukweli wenyewe na kutafuta suluhisho la kudumu.

Tunajidanganya kuahirisha jukumu hili mihimu kwa kudhani kuna mtu atakuja kufanya badala yetu. Tumezifinya hata fikra zetu na kushindwa kufikiri sawa sawa kutokana na kunywa nadharia mfu za elimu bandia zinazothibitishwa na vipimo bandia.

Wananchi tuamke tufanye mapinduzi katika elimu.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.