SEHEMU A
- Ni mambo yapi muhimu ya kuzingatiwa na mwalimu iwapo mbinu ya kualika mgeni itatumika?
- Eleza tofauti zilizopo kati ya kitabu cha kiada na ziada.
- Baadhi ya walimu hawapendi kufundisha kwa mbinu ya ziara. Unafikiri ni kwa nini?
- Taja vifaa vitano kwenye mkebe wa hesabu vitumikavyo katika elimu maumbo. Taja kazi ya kila kimoja.
- Taja zana tano za kufundishia Hisabati shule ya msingi.
- Kuna stadi ngapi za Hesabu? Zitaje.
- Mwalimu anatakiwa kuzingatia mambo gani wakati wa kuchagua mbinu ya kufundishia.
- Mbinu nzuri ya kufundishia ni ipi?
- Utamthibitishiaje mwanafunzi wa darasa la kwanza kuwa 3 + 5 = 8.
SEHEMU B
10. Muhtasari wa somo la Hisabati unatakiwa kuwa na sifa zipi?
Hisabati ni somo muhimu sana. Ni malengo yapi yanasababisha somo hili lifundishwe shule za msingi?
SEHEMU C
11. Zana za kufundishia zina umuhimu gani?
12. Ni mambo yapi yanayosababisha mbinu ya kufundishia kuwa nzuri au kuwa mbaya?
13. Eleza utakavyofundisha darasa la tatu (III) kuzidisha 3 kwa 5.
14. Eleza uhusiano uliopo kati ya njia za kufundishia, mbinu za kufundishia na mikakati ya ufundishaji. Toa mifano.
So fine but teacher u may put with its solns
LikeLike
samahani teacher tuta wezaje kupata marking schem ya maswali hayo ya hesabu. abby maurice ttc dar es saalam
LikeLike
MASWALI YAKO NI MAZUR SANA SASA JE NITAPATAJE MAJIBU YA MASWALI HAYA
LikeLike