Mbinu za Kufundishia Kiswahili – I

SEHEMU A 

  1. Taja mambo mawili unayoangalia ili mwanafunzi wako ayaweze unapomfundisha msamiati.
  2. Eleza unavyoelewa istilahi zifuatazo katika somo la Kiswahili;

a.Ufaraguzi
b.Kongamano
c.Tathimini
d.Msamiati

3. Eleza shabaha mbili (2) za kufundisha vitendawili katika shule za msingi.

4. Eleza sifa mbili (2) za Vitendawili.

5. (a) Maandalio ya Somo ni nini?
(b) Orodhesha vyanzo vitatu tu vya maandalio ya somo.

6. Ni mambo gani muhimu yanayosaidia kuzungumza na kusikiliza kuwepo (Misingi ya kusikiliza na kuzungumza). Taja manne (4) tu.

7. Eleza kwa kifupi mambo yanayofanyika katika ngazi ya matayarisho ya kufundisha kusoma.

8. Zipo sababu nyingi zinazofanya wanafunzi washindwe kusoma katika viwango mbalimbali. Ukirejea mtoto wa darasa la tatu, unafikiri sababu hizo ni zipi?
Taja sababu zinazotokana na mazingira ya shuleni.

9. Wewe kama mwalimu katika darasa la tatu unafikiri hati nzuri ni ipi?


SEHEMU B 

10. Eleza utafundishaje nahau ‘Unga mkono’ kwa mbinu ya maelezo katika darasa la sita.

11. Eleza Mazoezi matano (5) yafaayo kutolewa kwa wanafunzi wa darasa la saba baada ya kufundisha usimulizi wa hadithi Fulani.

12. Unapofundisha wanafunzi wa darasa la tano juu ya uandishi wa barua rasmi unatakiwa kuzingatia na kusisitiza juu ya mambo muhimu kumi (10) ili wayafahamu. Yataje.


SEHEMU C 

13. Fafanua sababu na hatua za kufundisha mwandiko katika darasa la kwanza..

14. (a) Lugha ni nini?
(b) Taja sifa zisizopungua sita za lugha yeyote ile.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Mbinu za Kufundishia Kiswahili – I

    1. Asante tutajitahidi kufanya hivyo, ila Mbinu zote zilivyo unaweza kuziboresha na kuzitumia kufundishia somo lako zaidi utambue unawafundisha watoto wa umri upi. Tutajitahidi sana kuzituma humu.

      Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.