Mbinu za Kufundishia Kiswahili – II

SEHEMU A 

  1. Taja mambo manne yanayoangaliwa wakati mwanafunzi anapofundishwa kusoma kwa sauti.
  2. Tunga sentensi moja moja kwa kutumia Nahau zifuatazo kuonesha dhana yake:

i) Moyo
ii) Tia fora
iii) Anika juani
iv) Bega kwa bega

3. Taja zana nne (4) unazodhani zinafaa kufundishia kusoma katika darasa la Pili.

4. Bainisha makundi manne ya Barua.

5. Kwa nini Somo la Imla hufundishwa katika Shule za msingi. Toa sababu mbili tu.

6. Kwa kutumia michoro ya mishale onesha utawafundishaje wanafunzi wa darasa la Kwanza kuandika herufi na namba zifuatazo:-

i) a
ii) 8
iii) s
iv) 5

7. Taja namna utakavyomwezesha mwanafunzi wa darasa la Kwanza kukuza Stadi ya kuzungumza.

8. Taja namna fasihi inavyojitokeza katika somo la Kiswahili katika Shule za Msingi.

9.  Ainisha maneno yaliyounda sentensi ifuatayo:- ‘Gari langu jana limeharibika vibaya sana sana’.


SEHEMU B 

10. Eleza hatua za kufuata katika kufundisha Utungaji (maelezo ya picha) ukitumia mbinu ya mazungumzo.

11. Eleza utafundishaji mada ya Ufahamu kwa wanafunzi wa darasa la nne lenye wanafunzi 60 huku ukiwa na vitabu sita vya kiada.

12. Fafanua matumizi ya Stadi ya Kuandika katika maisha ya kila siku ya kijana aliyehitimu vema Elimu ya Msingi.


SEHEMU C 

13. Eleza hatua za kufuata wakati wa kufundisha mada ya Kiswahili kwa kutumia mbinu ya Igizo.

14. ‘Uchaguzi wa mbinu nzuri ya kufundisha jambo Fulani katika Kiswahili, hutegemea sana vigezo mbalimbali avichunguzavyo Mwalimu wa somo’. Jadili.

15. Bainisha vipengele vyote muhimu vlivyomo kwenye andlio la somo

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Mbinu za Kufundishia Kiswahili – II

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.