Mbinu za Kufundishia Kiswahili – III

SEHEMU A 

  1. Taja malengo mawili ya kufundisha Kiswahili kwa wanachuo wa kozi ya ualimu daraja la A.
  2. Taja vifaa vya mtaala vya somo la Kiswahili viwili vinavyomhusu zaidi mwanafunzi wa shule ya msingi katika harakati za kujifunza somo hilo.
  3. Eleza matumizi mawili tu ya Muhtasari wa somo la Kiswahili kwa mwalimu afundishaye somo hilo katika shule za msingi.
  4. Taja stadi kuu nne za lugha ya Kiswahili kwa mfululizo au mpangilio wa ufundishaji na ujifunzaji wake.
  5. Andika methali tatu zinazofanana na hii ifuatayo; ‘Asiyesikia la mkuu huvunja guu’.
  6. Taja matumizi matatu ya kitabu cha kiongozi cha mwalimu wa somo la Kiswahili.

Andika ‘Kweli’ au ‘Uwongo’ kwa swali la 7 – 9.

 7. Mbinu za kufundishia na kujifunzia zifuatazo hazifai kufundishia Kiswahili, ziara na ‘majadiliano’.

8. Methali na Nahau zifundishwazo katika shule za msingi siyo vipengele vya kifasihi.

9. Mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule za msingi lazima azingatie malengo ya somo kwa wanafunzi wake kwamba ni kumuwezesha mwanafunzi kumudu kusikiliza, kuzungumza, kusoma, kuandika na kuhesabu katika Kiswahili.


SEHEMU B 

10. Taja na fafanua nyanja tatu za Elimu katika somo la Kiswahili.

11. Eleza muundo wa muhtasari wa somo la Kiswahili wa shule za msingi.

12. Eleza madhara yampatayo mwanafunzi afundishwaye na mwalimu bila kuwa na muhtasari wa somo la Kiswahili.


SEHEMU C 

13. Fafanua nadharia mbili zinazoelezea dhana ya kufundisha.

14. Kufundisha ni nini?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

6 thoughts on “Mbinu za Kufundishia Kiswahili – III

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.