Mbinu za Kufundishia Maarifa ya Jamii – I

SEHEMU A 

  1. Eleza kwa ufupi utakavyofundisha mada ya Mkutano wa Berlin 1884 – 85.
  2. Chagua mbinu moja ambayo hushughulisha wanafunzi katika tendo la kujifunza. Kisha Eleza hatua za kufuata unapotumia mbinu hiyo.
  3. Mada: Vita vya Maji maji 1905 – 7!

a. Ni mada ndogo itokayo na Mada kuu ipi?
b. Hufundishwa darasa lipi katika Shule ya Msingi?
c. Eleza jinsi unavyoweza kufundisha ukitaja zana na mbinu utakazotumia kufundishia mada hiyo.

4. Andaa maswali manne ya majadiliano kuhusu mada ya ujio wa Wareno katika Pwani ya Afrika mashariki.

5. Taja faida tatu za kuwa na Shajara la Somo.

6. Taja faida nne (4) za Muhtasari wa Somo la Maarifa ya Jamii.

7. Toa tofauti tatu (3) zilizopo kati ya Kitabu cha Mwanafunzi na Kiongozi cha Mwalimu.

8. Mada zifuatazo hufundishwa katika madarasa yapi katika Shule za Msingi?

a. Kilimo cha Mazao
b. Nishati
c. Haki na wajibu wa Raia
d. Ukoo

9. Taja matumizi ya Nguvu za Nyuklia.


SEHEMU B

10. Wanafunzi wengi hushindwa mtihani wa somo la Maarifa ya Jamii katika shule yako. Toa sababu unazofikiri zinasababisha hali hiyo na pendekeza muafaka wa suala hilo.

11. Thibitisha usemi kwamba mbinu ya majadiliano katika kufundisha somo la maarifa ya Jamii huwa na ufanisi mkubwa


SEHEMU C 

12. (a) Unaelewa nini juu ya Uvuvi haramu?
(b) Taja faida zisizopungua tano (5) za samaki katika nchi ya Tanzania.

13. Upatikanaji wa madini mbalimbali katika nchi ya Tanzania, yamewezesha nchi kupiga hatua katika nyanja mbalimbali. Jadili kauli hii.

14. Wewe kama Mwalimu wakati wa Mazoezi ya kufundisha (BTP) na ulifundisha darasa la VI, Jiografia, ainisha aina kuu tatu za miamba na Eleza sifa za kila aina kwa wanafunzi wako.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “Mbinu za Kufundishia Maarifa ya Jamii – I

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.