Mbinu za Kufundishia Maarifa ya Jamii – II

SEHEMU A 

  1. Andika faida tatu (3) za ujia shirikishi katika ufundishaji wa maarifa ya jamii.
  2. Chanzo kimojawapo cha uharibifu wa mazingira ni shughuli afanyazo binadamu, taja shughuli hizo tatu (3).
  3. Eleza ufanisi unaopatikana katika somo la Maarifa ya Jamii unapotumia mbinu ya majadiliano.
  4. Taja aina kuu nne (4) za mifumo ya jadi iliyokuwepo afrika mashariki kabla ya kuja wakoloni.
  5. Taja sifa za kiongozi bora shuleni.
  6. Toa maana ya Ujima,Ukabaila, Mtemi.
  7. Ujio wa Waarabu ni mada inayofundishwa darasa la tano. Andaa maswali manne (4) ya majadiliano kuhusu mada husika.
  8. Ainisha jumuiya kuu mbili (2) za kimataifa zinazoshirikiana na Tanzania.
  9. Eleza jinsi tawala za jadi zilivyogawana majukumu ukichukulia mfano wa wamasai.

SEHEMU B 

10. Eleza utafundishaje mada ya Hali ya hewa darasa la saba juu ya mada ndogo ‘Asili ya Mvua’ kwa mbinu ya jaribio.

11. (a) Majadiliano ni nini katika kufundisha na kujifunza?
(b) Eleza hatua za kufuata unapotaka kufundisha kwa mbinu ya majadiliano.

12. Fafanua madhara/mapungufu mawili na faida mbili za kufundisha kwa mbinu ya majadiliano.


SEHEMU C 

13. Tufe ni kifaa/zana inayofaa kufundishia somo la Jiografia katika shule za msingi. Bainisha ni mada zipi sita utafundisha kutumia tufe darasa la III – VII.

14. ‘Maadamu kuna muhtasari wa somo la Maarifa ya jamii basi hakuna haja ya kutumia kiongozi cha mwalimu cha somo katika tendo la kufundisha’, alisema mwalimu Kalimanzila.
Jenga hoja kumwonesha mwalimu Kalimanzila umuhimu wa kiongozi cha mwalimu cha somo.

15. Fikiria na kisha eleza matatizo utakayoyapata iwapo utafundisha somo lako bila kuwa na kitabu cha kiada cha mwanafunzi.
Madhara gani pia yatajitokeza kwa wanafunzi wako?

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.