Mbinu za Kufundishia Maarifa ya Jamii – III

SEHEMU A 

  1. Eleza maana ya dhana zifuatazo:-

a) Maarifa
b) Jamii

2. Andaa maswali manne ya majadiliano kuhusu mada ya ujio wa Wareno katika Pwani ya Afrika Mashariki darasa la tano.

3. Taja aina mbili ya zana ambazo unaweza kuzitumia wakati unapofundisha mada ya ‘Mfumo wa jua na sayari’.

4. Orodhesha faida nne za nukuu za somo kwa Mwalimu anapofundisha Somo la Maarifa ya Jamii.

5. Eleza matumizi manne ya tufe kwa Mwalimu wa Somo la Maarifa ya Jamii na Wanafunzi wake darasani.

6. Ni muhimu Mwalimu kuwa na Azimio la Kazi. Toa sababu nne kuthibitisha Usemi huo.

7. Ili lengo mahsusi liwe na ufanisi linahitaji kuonesha mambo fulani muhimu. Taja mambo matatu (3).

8. Eleza tofauti kati ya Kontua na mistari ya Latitudo.

9. Bainisha kati ya lengo la Jumla na lengo Mahsusi.


SEHEMU B 

10. Ramani ni moja ya zana utakazotumia mara kwa mara unapofundisha Somo la Jiografia. Eleza umuhimu wa zana za kufundishia na kujifunza.
Kisha waeleze wanafunzi wako wa darasa la IV mambo muhimu katika ramani.

11. Umejiandaa kufundisha mada ya kupatwa kwa mwezi katika Maarifa ya Jamii kwa kutumia onesho mbinu;

a) Taja zana muhimu utakazozitumia katika kufundisha mada hii
b) Eleza jinsi kupatwa kwa jua kunavyotokea.


SEHEMU C 

12. Ili kumaliza mapema ufundishaji wa mada zilizomo katika Muhtasari wa Maarifa ya Jamii Mwalimu anashauriwa atumie mbinu ya Mhadhara tu. Jadili.

13. Tathmini katika ufundishaji hufanyika kwa njia mbalimbali. Taja njia hizo na eleza umuhimu wa kila njia.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Mbinu za Kufundishia Maarifa ya Jamii – III

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.