Misingi ya Elimu – I

SEHEMU A 

  1. Oanisha mawazo yaliyoko katika ORODHA ‘B’ na yale yaliyoko kwenye ORODHA ‘A’ kwa kuandika herufi ya jibu kutoka ORODHA ‘B’ kando ya namba ya kipengele kutoka ORODHA ‘A’.

ORODHA   A

ORODHA   B

i. Michepuo ya Masomo   ilianza katika Elimu ya Sekondari
ii. Jukumu la kulipia gharama za Elimu ya msingi lilichukuliwa na   Serikali.
iii. Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu yalianzishwa.
iv. Upanuzi wa Elimu (Msingi, Sekondari na Vyuo) na kuondoa Ubaguzi wa   aina zote ulioachwa na Wakoloni.
v. Philips Stokes.
vi. Mahudhurio ya Elimu ya Msingi yalifanyika kuwa lazima kwa sheria.
a). 1969 – 1974
b). 1976
c). 1962
d). 1955
e). 1972
f). 1973
g). 1965
h). 1961 – 1964
i). 1924
j). 1978
k). 1979
l). 1864 – 1969

2. Orodhesha vigezo sita (6) vya Elimu linganishi.

3. Fafanua Philips Stokes wakati wa Utawala wa Waingereza.

4. Taja muundo wa Elimu wakati wa Utawala wa Wajerumani Tanzania bara.

5. Toa shabaha mbili (2) za Elimu katika Taifa lolote lile.

6. Taja Viongozi wawili (2) wa Elimu ngazi ya Kata.

7. Eleza majukumu mawili (2) tu ya mmoja wa viongozi wa Elimu Katani uliowataja katika swali la 6.

8. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi huteuliwa kutokana na sifa kadhaa. Taja sifa tatu (3) za Mwalimu Mkuu.

9. Eleza jinsi viongozi wakuu wawili (2) wa Kamati ya Shule wapatikanavyo.


SEHEMU B 

10. Jadili umuhimu wa mipango katika utoaji wa Elimu nchini Tanzania.

11. Falsafa ya Elimu ya kujitegemea iliweza kukidhi mahitaji ya Taifa letu katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi vya siasa. (Jadili).

12. Fafanua kwa kina mambo matatu (3) yaliyoagizwa na Azimio la Musoma katika kuimarisha Elimu nchini Tanzania.

13. Elimu ya Kujitegemea imejengwa katika misingi yake. Jadili misingi minne (4).


SEHEMU C 

14. Eleza faida sita (6) kwa shule ya msingi yenye Kamati ya Shule na madhara mawili (2) kwa shule isiyo na Kamati ya Shule.

15. (a) Taja kamati tano (5) za ushauri wa mwalimu.
(b) Fafanua majukumu matatu (3) ya moja ya Kamati ulizotaja katika 15 (a).

16. Eleza mambo akiyafanya mwalimu, yanaweza kuendeleza ubaguzi wa kijinsia shuleni.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

5 thoughts on “Misingi ya Elimu – I

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.