Misingi ya Elimu – II

SEHEMU A 

1. Toa maana ya istilahi zifuatazo;

a. Elimu
b. Maarifa
c. Mwelekeo

2. Bainisha tofauti iliyopo kati ya mtu mwenye elimu na mtu aliyeelimika.

3. Orodhesha malengo sita (6) ya muhtasari wa misingi ya elimu.

4. Eleza njia tano (5) za kupata elimu.

5. Nini maana ya Shule?

6. Eleza aina kuu nne za Viongozi na uongozi.

7. Taja tofauti nne zilizopo kati ya uongozi wa pamoja na na uongozi wa mahusiano mema.

8. Taja hasara tano (5) za uongozi wa kiimla. Kwa nini baadhi ya viongozi wa shule za msingi hupendelea mtindo huu wa uongozi?

9. Eleza majukumu ya mwalimu mkuu kuhusu mapato na matumizi ya fedha za shule.


SEHEMU B 

10. Fafanua malengo saba (7) ya mafunzo ya ualimudaraja la A.

11. Jadili aina za elimu na mifumo yake.

12. Jadili sifa nne (4) za Elimu rasmi.

13. jadili misingi mitatu (3) ya elimu ya jadi.


SEHEMU C 

14. Uongozi ni utoaji wa dira. Jadili dhana hiyo kwa kutumia mifano halisi kulingana na aina kuu nne za uongozi.

15. (a) Fafanua maana ya istilahi zifuatazo;

a. Uongozi wa shule
b. Uongozi

(b) Eleza tofauti iliyopo kati ya Utawala na Uendeshaji wa Shule ya msingi.

16. Fafanua mambo matano (5) yanayopelekea muingiliano wa majukumu kati ya Mwalimu mkuu na Kamati ya Shule.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Misingi ya Elimu – II

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.