Mitaala na Ufundishaji – I

SEHEMU A 

1. Toa ufafanuzi kuonesha tofauti kati ya mbinu zifuatazo za kufundishia;

a.Chemsha bongo
b.Bungua bongo
c.Maswali na Majibu

2. Utazingatia mambo gani wakati unaandaa nukuu za somo? Taja manne tu.

3. Orodhesha mambo muhimu yanayopaswa kuwepo katika Muhtasari wa Mafunzo kwa somo au kozi yoyote ile.

4. Taja vipengele vitano muhimu vinavyoonesha ukamilifu wa malengo mahsusi yaliyotajwa kiumwenendo.

5. Eleza kwa kifupi dhana zifuatazo;

a.Shajara la Somo/Batli
b.Kudhibiti darasa.

6. Wewe kama Mwalimu utazingatia mambo gani ili kudumisha nidhamu ya darasa unapokuwa ukifundisha?

7. Mawasiliano ya darasani ni muhimu sana katika mchakato wa kufundisha na kujifunza darasani. Je, utawezeshaje mawasiliano hayo?

8. Chunguza mchoro ufuatao kuhusu vipengele vya mtaala, kisha kamilisha kwa kutaja vipengele hivyo.

xA………………………………………………………………
B………………………………………………………………
C………………………………………………………………
D………………………………………………………………
E………………………………………………………………

 

 

9. Taja misingi mitatu (3) ya uchaguzi wa maudhui ya mtaala.


SEHEMU B 

10. Kwa vipi maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, Siasa/falsafa, mazingira na wakati vinachangia katika kupanga na kukuza mitaala ya Elimu?

11. Bainisha faida za kuandaa somo na madhara ya kutofanya hivyo.

12. Taja na fafanua makundi muhimu ya zana za kufundishia.


SEHEMU C 

13. Fafanua mambo ya kuzingatia na umuhimu ya kutumia mbinu ya ziara kwa darasa la Tano.

14. (a) Nini maana ya Tathmini ya Mtaala
(b) Eleza umuhimu wa kutathmini Mtaala.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

5 thoughts on “Mitaala na Ufundishaji – I

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.