Mitaala na Ufundishaji – II

SEHEMU A 

1. Taja ngazi nne (4) za elimu unazozifahamu.

2. Tofautisha njia na mbinu za kufundishia na kujifunzia.

3. Taja sifa za njia ya muhadhara kwa wanafunzi ambao ni watu wazima.

4. Je, unafikiri tunaposema “Mtaala” tuna maana ya mambo yapi? Taja mambo nane (8) tu.

5. Taja matumizi manne (4) ya mtaala kwa walimu.

6. Mtaala una malengo makuu matatu. Taja malengo hayo.

7. Taja masomo manne (4) tu yanayofundishwa shule za msingi nchini.

8. Taja vyanzo vinne (4) vya mtaala.

9. Taja aina nne (4) ya wanafunzi wanaostahili kuandaliwa mtaala.


SEHEMU B 

10. Kuna usemi usemao; baadhi ya walimu wetu hawazimudu vizuri mada wanazofundisha. Kwa hali halisi ya ufundishaji katika shule zetu nyingi hairidhishi. Jadili usemi huu kwa hoja nne tu.

11. Jadili changamoto tano (5) zinazoikabili mitaala ya elimu nchini.

12. Uchaguzi wa njia/mbinu za kufundishia na kujifunzia hutegemea mambo mengi.
Jadili mambo ya kuzingatia wakati wa kuchagua mbinu za kufundishia na kujifunzia.
Kwa maoni yako unafikiri ni mbinu ipi inafaa kufundishia na kujifunzia. Toa sababu kwa jibu lako.

13. Mtaala ni dhana pana. Jadili kauli hii.


SEHEMU C 

14. Mitaala ni silaha ya ukombozi katika jamii. Jadili kauli hii ukidhihirisha umuhimu wa dhana ya mitaala katika jamii (tumia hoja sita (6) tu).

15. Ukosefu wa sera thabiti inayosimamia utekelezaji wa yale yaliyomo kwenye mfumo wa elimu ndio chanzo kikuu cha Mitaala yetu kuonekana haifai.
Jadili kauli hii na jaribu kuishauri serikali ili kuiboresha mitaala yetu.

16. Jadili ngazi tatu zinazotumika kuchanganua mtaala. Ngazi zote zielezwe kwa kina.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Mitaala na Ufundishaji – II

  1. mpo vizur nimependezwa nazo sana hasa Maswali mengi namazuri yanayonijengea stadi na maarifa wakati wakujibu mitihani yangu ya ualimu pia nimefunguka kwa upana zaidi

    Like

  2. Nimeona ipo poa na hongereni kwa kutoa maswali ya changamoto kiasi hiki kwa kuboresha walimu WA awali pia na walimu WA ngazi tofauti tofauti, big up guys

    Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.