Sayansi – I

SEHEMU A 

1. Nishati ni nini? Zitaje aina za nishati unazozifahamu.

2. Eleza maana ya mbinu za kufundishia na kujifunzia.

3. (i) Taja magonjwa 5 yanayoweza kushambulia viungo vya uzazi kama usafi wa mwili utakuwa duni.  (ii) Eleza jinsi unavyoweza kufundisha usafi wa viungo vya uzazi (zingatia mpangilio wa andalio la somo).

4. Taja hali za maada na eleza sifa za maada katika kila moja ya hali hizo.

5. Eleza kwa kutoa mfano tofauti kati ya mabadiliko ya maada kiumbo na kikemikali.

6. Kuna Daraja ngapi za nyenzo? Zitaje.

7. Orodhesha malengo mahususi yasiyopungua mawili kwa kila mada zifuatazo;

a. KUKUA
b. KUJONGEA
c. KUITIKIA VICHOCHEO
d. UZAZI
e. UTOAJI TAKA MWILI

8. Taja vyanzo mbalimbali vya nishati.

9. Bainisha athari nne za matumizi mabaya ya somo la kemia.


SEHEMU B 

10. (i) Eleza tofauti iliyopo kati ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
(ii) Bainisha tabia, mila na desturi zisizopungua kumi (10) zinazochangia kueneza magonjwa ya kuharisha, kuhara, minyoo ya safura, funza, upele, ukoma, trakoma, siko seli, utapia mlo na fistula.

11. Eleza utakavyoshawishi wanafunzi wako wakubaliane na wewe kuwa kani za sumaku zaweza kupenya mada si sumaku.

12. Buni jaribio utakalotumia kuongoza wanfunzi wa darasa la 6 wagundue kuwa ‘hewa ni maada’.


SEHEMU C 

13. Eleza jinsi unavyoweza kutumia njia ya kazi mradi kwa kufundishia somo la mabadiliko ya maada ya kiumbo.

14. (i) Eleza maana ya uainishaji wa viumbe hai.
(b) Baini dola kwa viumbe vifuatavyo;
Uyoga na mapunye, jongoo na katani.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

8 thoughts on “Sayansi – I

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.