Sayansi – II

SEHEMU A 

1. Taja kazi za sehemu zifuatazo katika mwili wa binadamu;

Sehemu

Kazi

(a). Ngozi  

(a)……………………………….
(b)……………………………….

(b). Uke  

(a)……………………………….
(b)……………………………….

(b). Uume  

(a)……………………………….
(b)……………………………….

2. Bainisha magonjwa yanayoweza kumshambulia mtu asiyefanya usafi wa;

i. Nywele
ii. Masikio
iii. Ngozi
iv. Macho

3. Taja mbinu nne (4) zinazofaa kufundishia kazi za sehemu za nje za mwili wa binadamu.

4. Njia za kufundishia na kujifunzia sayansi ziko nyingi sana, lakini zaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili. Taja makundi hayo; na kwa kila kundi toa mifano miwili.

5. Nini maana ya kujifunza?  Taja vitendo vitatu (3) vinavyoweza kumwonesha mwalimu wa sayansi kuwa wanafunzi wake wanajifunza wakati wa kipindi chake.

6. Inapobidi mwalimu kufundisha sayansi kwa njia ya mhadhara hana budi kuhusisha na mambo mengine ili wanafunzi waweze kuelewa anachofundisha na wasichoke. Taja mambo manne tu.

7. Walimu wengi wa sayansi katika shule nyingi nchini hupenda kufundisha kwa njia ya mhadhara kutokana na imani potofu. Taja imani nne (4) tu.

8. Mtaala wa sayansi ni nini?

9. Taja vifaa vya Mtaala wa Sayansi kwa shule za msingi.


SEHEMU B 

10. Muhtasari wa somo la Sayansi unatakiwa kuwa na sifa zipi?

11. Tunga beti mbili za shairi, wimbo au ngonjera kuhusu magonjwa ya kuambukizana na namna ya kujikinga na magonjwa.


SEHEMU C 

12. Bainisha tofauti zilizopo kati ya kitabu cha kiada na kitabu cha ziada.

13. Eleza hatua utakazofuata kudhihirisha kuwa mwanga husafiri katika mstari ulionyooka.

14. Eleza umuhimu wa kufundisha somo la biolojia katika shule za msingi.

15. Ni vitendo vipi kati ya hivi, vinaonesha kwamba mwalimu wa sayansi anafundisha kwa ufanisi? Weka alama ya (√) sehemu inayohusika baada ya kufanya uchunguzi wako.

 

KITENDO

CHA   KUFUNDISHA

SIYO   CHA KUFUNDISHA

i.Mwalimu   anazungumza na wanafunzi darasani …………… ……………
ii.Mwalimu anaandika   ufupisho wa somo ubaoni …………… ……………
iii.Mwalimu anawauliza   wanafunzi maswali …………… ……………
iv.Mwalimu anachora   vielelezo ubaoni …………… ……………
v.Mwalimu anawapiga   wanafunzi baada ya kushindwa kujibu swali …………… ……………
vi.Mwalimu   ananakilisha ubaoni …………… ……………
vii.Mwalimu   anawakaririsha wanafunzi …………… ……………
viii.Mwalimu anawafokea   wanafunzi …………… ……………
ix.Mwalimu anachagua mwanafunzi   mwenye uwezo kuwafundisha wanafunzi wengine darasani …………… ……………
x.Mwalimu   anasahihisha kazi za wanafunzi na kurejesha kwa masahihisho …………… ……………
xi.Mwalimu anamchagua   mwanafunzi kusimulia hadithi darasani …………… ……………
xii.Mwalimu anaigiza   mbele ya darasa …………… ……………

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Sayansi – II

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.