Stadi za Kazi – I

SEHEMU A 

1. Eleza kwa kifupi faida nne (4) za mwanafunzi wa shule ya msingi kujifunza somo la Stadi za Kazi.

2. Nini maana ya Istilahi zifuatazo;

a. Kilimo
b. Riadha
c. Uashi
d. Ufundi Mchundo

3. Taja aina nne (4) za michezo ya asili.

4. Orodhesha aina nne (4) za matofali.

5. Taja rangi tatu (3) za msingi katika usanii wa picha.

6. Orodhesha viambaupishi vinne (4) vya sambusa.

7. Orodhesha vipengele vinne (4) vya stadi kuu ya Sayansi Kimu.

8. Mlo kamili na bora ni Chakula cha aina gani?

9. Tofautisha upishi wa kukaanga na kuchemsha.


SEHEMU B 

10. Baadhi ya watu huamini kuwa kufuna nguo na kuzipiga pasi mara kwa mara huchakaza nguo. Thjibitisha usemi huu.

11. Fafanua maneno yafuatayo kwa maelezo mafupi;

a. Upishi
b. Udobi
c. Ushoni
d. Ufumaji


SEHEMU C 

12. Ususi ni stadi inayotangaza utamaduni wa jamii na vilevile kuwapatia watu ajira na kuwaongezea kipato, hivyo kupunguza umaskini. Thibitisha kauli hiyo.

13. Taja na Eleza faida tano (5) na hasara tano (5) za ufugaji huria.

14. Sekta ya kilimo imekuwa ikitiliwa mkazo sana nchini. Lakini imeshindwa kufanikiwa kutokana na matatizo kadhaa yanayoikabili. Jadili.

15. Katika karakana ya useremala inaweza kutokea ajali kama vile moto au kuumia. Eleza kwa kifupi vyanzo vya ajali hizo.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

6 thoughts on “Stadi za Kazi – I

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.