Stadi za Kazi – II

SEHEMU A 

1. Eleza kwa kifupi maana ya istilahi zifuatazo;

a. Stadi za kazi
b. Zana

2. Taja malengo manne (4) ya somo la stadi za kazi.

3. Taja vipengele vinne (4) vinavyofundishwa katika sanaa za ufundi.

4. Katika darasa la V – VII kila mwanafunzi anatakiwa kusoma staid za kazi tatu, ikiwemo elimu ya viungo na michezo kwa nini?

5. Taja makundi makuu matatu ya nguo tunazovaa.

6. Taja vifaa muhimu katika stadi ya udobi.

7. Taja njia unazoweza kutumia kutambua nguo za aina mbalimbali.

8. Nini maana ya istilahi zifuatazo;

a. Uchoraji
b. Stenseli
c. Kusana picha

9. Orodhesha fani mbili za usanii wa picha, na kwa kila fani eleza kwa kifupi inahusu nini.


SEHEMU B 

10. (a) Kwa nini unapaswa kuchora miraba unapochora herufi? (b) Ni herufi zipi zinazochukua nafasi kubwa na ndogo zaidi katika miraba kuliko zingine.

11. Eleza hatua utakazofuata wakati wa kufua nguo za pamba za rangi.


SEHEMU C 

12. Fafanua hatua tatu (3) utazotumia kabla ya kusana picha.

13. Kuna umuhimu gani kuzigawa nguo katika mafungu kabla ya kufuliwa.

14. Eleza umuhimu wa kutumia zana na vifaa katika ufundishaji.

15. somo la stadi za kazi linahitaji mwalimu bingwa na mwenye uwezo wa kutumia Mbinu na Njia Shirikishi. Eleza ni kwa nini?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

12 thoughts on “Stadi za Kazi – II

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.