STADI ZA KAZI – Sanaa za Maonesho

watoto2Sanaa ni nini?

 • Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa.
 • Sanaa ni kioo cha jamii

Nadharia hii inaonesha kuwa kazi ya sanaa ni kutoa taswira ya jinsi ilivyokuwa jamii/kitu Fulani.

Sanaa za Maonesho ni pamoja na;

 • Tamthilia,
 • Hadithi,
 • Mashairi,
 • Ngonjera,
 • Ngoma
 • Muziki nk.

TAMTHILIA

Michezo ya kuigiza ni jina ambalo lilikuwa likitumika kuelezea Tamthilia. Neno “Michezo ya Kuigiza” halitoi picha nzuri kwa sababu matukio au hadithi yoyote tayosimuliwa huonekana kama mzaha tu.

Lakini neno “TAMTHILIA” hutia msisitizo kuwa ni hadithi iliyobuniwa au kutolewa kwa lengo la kueleza dhamira Fulani kwa njia ya vitendo na maneno mbele ya hadhira.

Tamthilia hii hukamilika endapo tu itaoneshwa mbele ya Hadhira.

Muigizaji wa tamthilia anatakiwa kushirikiana na hadhira moja kwa moja kwa kupitia hisia, ishara, au vitendo vyake katika igizo linalohusika.

AINA ZA TAMTHILIA

Kuna aina kuu nne za Tamthilia;

TANZIA

Tamthilia hizi hujengwa na visa, vituko na migogoro na hatma yake  ni kifo kwa muhusika mkuu au jamii. Hii huonekana mwisho wa mchezo.

FUTAHI

Tamthilia hizi hujengwa na  visa, vituko na migogoro ambayo huishia kwenye furaha na ushindi.

YUGA

Ni Tamthilia ambazo huonesha furaha na huzuni kwa wakati mmoja na kuwafanya watazamaji wafurahie vichekesho vilivyomo.

RANSA

Yahusu utani na kusahihishana au kejeli na mzaha wa ukweli wa maisha. Tamthilia hukamilika endapo zitaoneshwa mbele ya watazamaji.

WAHUSIKA KATIKA TAMTHILIA

Wanaoigiza tamthilia ndio wahusika wakuu. Wahusika hawa wanaweza kuwa;

 • Watu
 • Wanyama
 • Mimea
 • Mizimu

Ilimuradi wapewe uhai kulingana na igizo lenyewe. Wahusika wanatakiwa kujipambanua au kueleza husika zao kwa kutumia mwili, mazungumzo na matendo.

Kuna aina mbili za wahusika katika Tamthilia;

–      Wahusika Wakuu

–      Wahusika Wadogo

Wahusika wakuu ndio wanaopeleka igizo mbele kutokana na kitendo au vitendo

PLOTI

Tamthilia husimuliwa kwa njia ya vitendo vikiambatana na maneno. Tamthilia pia husimuliwa kwa kufuata mtiririko na kutoa picha ya matukio na visa mbalimbali vikiwa ninabebwa na wahusika kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Mfululizo huo wa visa na matukio huitwa PLOTI.

Ploti hujengwa na sehemu kuu tatu nazo ni;

 • Mwanzo – ni utangulizi unaotolewa kuhusu wahusika, mwanzo n.k;
 • Kati – hubainisha ukweli kuhusu mhusika, tabia, vitendo, na mwenendo na maingiliano ya wahusika. Sehemu ya kati hufanya Hadhira ianze kupata picha halisi ya mchezo hivyo kufanya hadhira kuanza kutabiri mwisho wa mhusika au wahusika;
 • Mwisho – huonesha jinsi mhusika au wahusika wanavyofurahia au kuhuzunika kwa sababu ya ushindi au kifo cha mhusika

MGOGORO

Migogoro ni hali ya ukinzani baina ya vitu viwili au zaidi. Kwa kawaida tamthilia yeyote hubeba aina mbalimbali za mgogoro ili kuleta maana halisi ya masimulizi na vitendo.

Migogoro hiyo ndiyo inayofanya hadithi fulani iendelee na kuleta utamu wa kusanii.

MAUDHUI (DHAMIRA)

Maudhui ni mambo yote ambayo yamebeba matukio na vitendo katika tamthilia. Tunaweza kupima nafasi ya tamthilia katika jamii kutokana na maudhui yake.

Aidha Maudhui ni kiini cha matukio au visa vinavyotokea katika tamthilia. Kutokana na dhamira kuu twaweza kugundua dhamira ndogo ndogo.

Tamthilia yapaswa kuwa na maudhui yanayoibua hisia za kuleta mabadiliko katika jamii ingawa pia yaweza kutia hamasa ya kutambua wajibu wa kila mwanajamii.

MATUMIZI YA JUKWAA

Tamthilia itakamilika ikiwa itaoneshwa mbele ya watazamaji na sio kubaki katika maandishi tu.

Mara nyingi tamthilia huoneshwa katika jukwaa. Hivyo basi itafaa kujua umuhimu na matumizi ya jukwaa.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “STADI ZA KAZI – Sanaa za Maonesho

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.