Uraia – I

SEHEMU A 

1. Eleza maana ya istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika somo la Uraia;

a. Serikali Kuu
b. TEHAMA
c. Taifa
d. Ufisadi

2. Taja malengo manne (4) ya utamaduni wa kikoloni.

3. Taja ngazi/mfumo wa Mahakama za nchi ya Tanzania ukianzia ngazi/mfumo wa juu kwenda chini.

4. Eleza maana ya ulevi na utaje aina za ulevi.

5. Eleza umuhimu wa vyombo vya dola katika nchi yeyote.

6. Eleza jinsi haki za binadamu zinavyoweza kuvunjwa.

7. Taja Taasisi/Wizara zisizopungua nne (4) zilizo kwenye Serikali ya Muungano.

8. Orodhesha nyanja tano (5) za utamaduni wa kigeni.

9. Taja madawa ya kulevya yasiyopungua matano (5).


SEHEMU B 

10. Kila nchi huheshimiwa kutokana na utamaduni wake. Watanzania wanajivunia tamaduni zipi zisizo na kasumba yeyote ya ukoloni? Taja tamaduni 10.

11. ‘Vyombo vya habari katika mfumo wa utawala wa kidemokrasia vina umuhimu wake’. Jadili hoja hii kwa kuainisha kazi za vyombo vya habari zisizopungua nne (4) katika kuleta maendeleo katika mfumo huu wa kitawala.

12. ‘Dini za kigeni zimeleta ubaguzi’. Jadili athari hasi za madhehebu ya dini.


SEHEMU C 

13. ‘Nchi ya Tanzania siyo maskini ila Umaskini wake husababishwa na ufisadi wa vigogo walioko nchini’. Jadili kauli hii.

14. ‘Chaguzi nyingi katika Bara la Afrika, sio huru na za haki’. Kanusha au kubaliana na kauli hii kwa kuzingatia chaguzi za Kenya na Zimbabwe.

15. ‘Kujiuzulu kwa Viongozi mbalimbali kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma na utawala mbovu sio suluhu la kuleta utawala bora Tanzania’. Jadili kauli hii.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

8 thoughts on “Uraia – I

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.