MEI MOSI 2013 – Tujitafakari katika Kufanya Kilicho Sahihi

Tunawatakia Watumishi wote Sherehe Njema ya Mei Mosi
Tunawatakia Watumishi wote Sherehe Njema ya Mei Mosi

Ili nchi iwe na maendeleo ni muhimu kwa kila mwananchi adhamirie kufikia kiwango cha juu cha uadilifu. Hii ina maanisha kwamba kufanya kilicho sahihi daima ili kujenga amani ya watoto wetu, watumishi wenzetu na wananchi wengine.

Kama mtumishi wa umma, ili kufanya kilicho sahihi hapana budi kutekeleza majukumu kwa kuzingatia utaalamu, kuwa mwaminifu na kuwajibika. Kwa upande wake serikali ina jukumu la kuwajengea uwezo watumishi wake ili waweze kuzingatia utaalamu wao, wawe waaminifu na wawajibike.

Kufanya kilicho sahihi maana yake nini?

Kufanya kilicho sahihi ni kuzingatia utaalamu, kuwa mwaminifu na kuwa mwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kazi yako.

Hivyo tunahitaji kuwa na tabia ya uthubutu, tusikae kimia huku tukiugulia mioyoni kwa mambo tunayofanyiwa na watumishi wasio waadilifu.

Hivyo ukimwona mwananchi au mtumishi mwenzako anakiuka maadili ya utumishi wa umma unawajibika kutoa taarifa kwa Mamlaka inayohusika.

TUNAWATAKIA SIKU NJEMA YA MEI MOSI.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.