Ualimu – Maswali ya Kujipima | Siku 5 Kabla Mtihani wa GATCE

 1. Jadili nafasi ya mazingira katika kuimarisha au kukwamisha kujifunza kwa mtoto.
 2. Je, kazi ya ualimu ina sifa zipi za kimsingi za kuitwa kazi ya Kiutaalamu?
 3. Kuna umuhimu gani wa kujifunza kwa kuhusianisha vitu?
 4. Taja na eleza kanuni kuu nne za kujifunza.
 5. Kwa kutumia mifano, taja makundi makuu matatu ya Zana za Kufundishia.
 6. Kwa nini watoto hujifunza zaidi kupitia milango ya maarifa kuliko watu wazima?
 7. Kujifunza huimarika kwa kuzingatia Nyanja kuu tatu. Zitaje.
 8. Kwa kila Nyanja uluioitaja, eleza inahusiana na nini na vipi mwalimu anaweza kuiendeleza?
 9. Taja faida tano za maswali yanayoulizwa na mwalimu darasani.
 10. Eleza majukumu manne ya Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC).
 11. Eleza jinsi wanakijiji wanavyoweza kushirikishwa katika utoaji wa elimu shuleni.
 12. Taja na fafanua matatizo yanayowakabili walimu huko vijijini.
 13. Eleza mambo muhimu yanayopaswa kuwepo ili kufanikisha mazingira bora ya kazi.
 14. Mazingira duni ya nyumbani nay a shuleni yanaathiri ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili. Toa mifano ya mazingira duni ya nyumbani.
 15. Eleza maana ya makuzi ya mtoto.
 16. Taja vipengele mbalimbali vya kukua kwa mtoto.
 17. Eleza jinsi kukomaa kwa viungo vya mwili kunavyotegemeana na Mazoezi katika utendaji.
 18. Fafanua jinsi ambavyo viungo vya mtoto hutofautiana katika ukuaji.
 19. Eleza tofauti iliyopo kiakili kati ya mtoto wa miaka 2 – 4 na Yule wa miaka 12 – 15.
 20. Lugha ni nini?
 21. Taja viathiri vikuu viwili vinavyohusika katika kuamua hali na ukuaji wa mtoto.
 22. Eleza mchango wa kila kiathiri katika haiba ya mtu.
 23. Eleza ni kwa jinsi gani mambo yafuatayo yanavyoweza kuwa na matokeo chanya na hasi katika ukuaji wa mtoto kiakili na kimwili.
  1. Hali nzuri ya uchumi ya wazazi.
  2. Mtoto pekee katika familia.
 24. Tofautisha uchunguzi wa makini wa majaribio na uchunguzi wa makini usio wa majaribio.
 25. Kukua na kukomaa kwa mtoto kijamii hutegemea sana mchango wa walezi mbalimbali wanaoshirikiana na wazazi.
  1. Taja walezi watatu na fafanua jinsi kila mmoja anavyoweza kumsaidia mtoto kukua katika fani hii.
  2. Eleza kwa ufupi jinsi urafiki na uhasama vinavyotokea watoto wakati wanapokua.
 26. Bainisha vipindi vitano vya ukuaji wa mtoto kiakili kama vilivyoainishwa na mwanasaikolojia Jean Peaget.
 27. Kwa kila hatua bainisha tendo moja linalodhihirisha kukua kiakili.
 28. Nini maana ya lugha? Jadili hatua nne za ukuaji wa lugha.
 29. Jadili hitilafu 3 za kuzungumza wanazopata watoto.
 30. Kwa mujibu wa Hurlock, michezo ni nini?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

8 thoughts on “Ualimu – Maswali ya Kujipima | Siku 5 Kabla Mtihani wa GATCE

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.