Elimu ya Awali | MASWALI NA MAJIBU | Sehemu ya Kwanza

  1. Taja vifaa vitatu vya mtaala wa elimu ya awali unavyovifahamu.
  • Muhtasari wa vitendo vya masomo

Mwalimu atatumia muhtasari wa vitendo vya masomo kuandaa Azimio la Kazi na Andalio la Somo ya vitendo vya masomo. Pia mbinu za kufundishia na vifaa vitakavyotumka kufundisha mada za vitendo mbalimbali vya masomo.

  • Vitabu vya kiada na ziada
  • Vifaa vya kufundishia
  • Kiongozi cha mwalimu

Kumbuka

Mara nyingi tunafikiri mitaala ni kile kinachofundishwa darasani. Tunafikiri orodha ya masomo na silabasi. Fikra hizi siyo sahihi kwa shule za awali. Katika shule za awali mitaala ni mambo yote yanayotokea shuleni kila siku. Mawazo yetu ya mitaala ya elimu ya awali lazima yazingatie namna watoto wadogo wanavyojifunza. Wanajifunza kwa kutumia uzoefu wao wa kila siku, wanajifunza kwa kuangalia na kuiga wengine kwa kujaribu na kugundua kwa kushughulika na vitu halisi na kwa kucheza. Wanajifunza kama sehemu ya kukua kwao kwa jumla kunakojumuisha kiakili, kimwili na kijamii. Mtot mdogo hatofautishi baina ya wakati wa darasa na nje ya darasa, wakati wa kujisaidia au wa kunywa uji. Wote huo ni wakati wa kukua kwa mtoto, kwa hiyo yote hayo ni sehemu ya mitaala.

2. Eleza umuhimu wa kutumia vifaa vya mtaala katika kufundisha elimu ya awali.

Umuhimu wa kujua vifaa vya mtaala ni kumsaidia mwalimu wa elimu ya awali kupanga masomo yake vizuri na kufundisha kwa ufanisi kwa kufuata mpangilio aliopanga. Pia vinamsaidia kujua vifaa na zana gani aandae kwa ajili ya kufundisha mada mbalimbali.

3. Ufaraguzi wa zana za kufundishia na kujifunzia ni nini?

Kufaragua ni kubuni na kutengeneza zana husika kwa kutumia maarifa na ujuzi wa mwalimu au mtoto kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira ya shule.

4. Taja mambo yanayopimwa katika elimu ya awali.

  1. Maendeleo ya jumla ya mwanafunzi
  2. Bidii ya mwanafunzi
  3. Uwezo wa mwanafunzi

5. Tofautisha muhtasari wa elimu ya awali na wa shule za msingi.

Muhtasari wa elimu ya awali ni tofauti na ile ya shule za msingi kwa sababu umeundwa kwa vitendo vya masomo mbalimbali. Ni rahisi zaidi kuwafundisha watoto wadogo kwa vitendo zaidi kwa kuwa wanchoka haraka na uwezo wao wa kukaa muda mrefu na kumsikiliza mwalimu ni mdogo, hivyo kufundisha kwa njia ya vitendo kunawasaidia kulipenda somo na kuelewa kwa urahisi zaidi.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Elimu ya Awali | MASWALI NA MAJIBU | Sehemu ya Kwanza

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.