Ufundishaji – Maswali ya Kujipima | Siku 5 Kabla Mtihani wa GATCE

 1. Taja vitendo vinavyoonesha kuwa kujifunza kumefanyika.
 2. Taja mambo yanayoweza kumfanya mwanafunzi asijifunze.
 3. Fundisha walimu wenzako somo Fulani kwa kutumia njia ya maonesho.
 4. Ubora wa njia yeyote unategemea mambo gani? Eleza hatua kwa hatua namna ya kufanya jaribio lolote ili wanafunzi waweze kuelewa.
 5. Hadithi nzuri ina sifa zipi?
 6. Eleza hatua za kufuata wakati unapotaka kutatua tatizo lolote.
 7. Hakuna njia moja tu inayokidhi haja zote za kufundisha. Mwalimu fanisi ni Yule anayeweza kutumia njia zaidi ya moja wakati anapofundisha mada au somo lolote. Fafanua
 8. Ukosefu wa vyumba vya madarasa vya kutosha husababisha walimu kutumia mhadhara wakati wa kufundisha. Fafanua na toa mifano.
 9. Kazimradi ni njia ya kufundisha ambayo huwafunza walengwa kushirikiana. Fafanua na toa mifano.
 10. Nini maana ya “Zana ya Kufundishia”?
 11. Taja aina tatu (3) za zana za kufundishia.
 12. Eleza maana ya dhana. Toa mifano kusaidia ufafanuzi wako.
 13. Sufuri ni dhana muhimu katika Hisabati. Eleza utakavyofundisha dhana hiyo.
 14. Tunapofundisha dhana yeyote tunaanza kufundisha dhana rahisi kwenda ngumu. Toa mifano halisi.
 15. Dhana nyingi zinazofundishwa darasani ni dhahania. Chagua dhana mbili dhahania na ueleze jinsi utakavyofundisha dhana hizo ili watoto waelewe.
 16. Eleza manufaa ya kutumia zana wakati wa kufundisha.
 17. Taja malengo ya kuuliza maswali katika hatua ya;
  1. Utangulizi;
  2. Maarifa mapya;
  3. Kukaza maarifa.
 18. Tunga maswali yanayopima ngazi ya juu ya maarifa.
 19. Wanafunzi wanatofautiana katika Nyanja nyingi. Taja Nyanja hizo.
 20. Eleza hatua utakazochukua utakapomwona mtoto ana matatizo katika somo Fulani.
 21. Mwanaelimu mmoja alisema “Kila mtoto anaweza kujifunza.” Tetea au pinga usemi huu kwa kutoa sababu.
 22. Mazoezi mazuri yanapima kiwango cha wanafunzi kuelewa mada au somo analojifunza. Jadili.
 23. Kuna manufaa gani kwa mwalimu kuwapa wanafunzi kazi za kufanya nyumbani?
 24. Kujifunza ni mabadiliko ya kudumu katika mwenendo na hutokana na uzoefu. Jadili
 25. Eleza na fafanua nadharia ya “Umwenendo”.
 26. Toa mifano halisi darasani au maishani kuonesha kuwa mtoto hawezi kujifunza mpaka amefikia au amepata utayari Fulani.
 27. Eleza maana ya usemi huu, “Motisho huongeza tija.”
 28. Kwa nini mwanafunzi hufundishwa stadi ya kuzungumza kabla ya kumfundisha stadi ya kuandika?
 29. “Mazoezi huleta ubingwa”. Fafanua kauli hii.
 30. Tunaposema Fulani ana maarifa tuna maana gani?

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.