Jipime | Maswali 100 Wikiendi hii | Misingi ya Elimu

1. Eleza maana ya “ELIMU”

2. Taja sifa za mtu aliyeelimika.

3. Taja na fafanua njia kuu tatu za kupata elimu.

4. Taja na fafanua madhumuni manne ya elimu ambayo yanakidhi nchi zote duniani.

5. Chagua madhumuni matano kati ya madhumuni ya elimu Tanzania, na fafanua manufaa ya kila moja kati ya hayo.

6. Fafanua mfumo rasmi wa elimu ya Tanzania.

7. Taja na fafanua sifa tano za mfumo rasmi wa elimu.

8. Eleza maana ya mfumo wa elimu usio rasmi.

9. Eleza tofauti iliyopo kati ya mfumo rasmi na mfumo usio rasmi wa elimu.

10. Eleza maana ya madhumuni ya Elimu ya Jadi.

11. Taja na fafanua sifa kuu tano za Elimu ya Jadi.

12. Fafanua maarifa na stadi zilizofundishwa katika mitaala ya elimu ya Jadi.

13. Jadili mwenendo mwema na maadili yaliyokuwa katika mitaala ya Elimu ya Jadi.

14. “Katika elimu ya Jadi, baadhi ya mambo waliyofundishwa wavulana yalitofautiana na mambo waliyofundishwa wasichana” Jadili usemi huo.

15. Elimu ya jadi ilifuata mitaala gani?

16. Tanganyika (Tanzania Bara) iliwahi kutawaliwa na Waarabu, eleza kwa ujumla madhumuni manne ya wakoloni hao.

17. Taja na fafanua sifa tano za elimu ya shule za wamisionari.

18. Taja na jadili shabaha nne za elimu ya Wajerumani.

19. Ainsha mitaala iliyotumika katika elimu wakati wa ukoloni wa Kijerumani.

20. Elimu ya wakoloni wa Kiingereza ilikuwa na madhumuni gani?

21. Eleza tofauti za mifumo ya elimu wakati wa ukoloni wa kijerumani na wakati wa ukoloni wa kiingereza.

22. Eleza kasoro tano zilizojitokeza katika elimu ya kikoloni.

23. Taja na fafanua misingi mitatu mikuu ya Elimu ya Kujitegemea.

24. Elimu ya Kujitegemea ilikuwa na malengo gani?

25. Eleza mabadiliko ya mitaala yaliyotokana na falsafa ya Elimu ya Kijutegemea.

26. Eleza mambo makuu matano yaliyobuniwa na kutekelezwa chini ya mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya elimu: 1969 – 1974.

27. Taja na fafanua mambo muhimu matano yaliyoagizwa katika Azimio la Musoma.

28. “Elimu ya Msingi ni elimu kamili na inayojitosheleza”. Fafanua usemi huu kwa kutoa mifano ya kutosha.

29. Eleza uhusiano uliopo kati ya Azimio la Arusha na Azimio la Musoma kuhusu mambo ya kielimu.

30. Azimio la Musoma liliainisha matatizo gani ya kieleimu?

31. Eleza maana na madhumuni ya Elimu ya Awali.

32. Kuna tofauti gani kati ya mitaala ya Elimu Awali na ile ya Shule za Msingi?

33. Eleza athari za kutumia adhabu ya viboko na hasira kuwarekebisha watoto wa chekechea.

34. Mitaala ya Elimu Awali imeandaliwa KIVITENDO, bali ile ya Elimu ya Msingi imeandaliwa KIMASOMO. Jadili hoja hiyo.

35. Taja na fafanua aina sita za ulemavu unaoweza kuwapata watoto wadogo.

36. Eleza jinsi utakavyowatambua darasani watoto wenye ulemavu mbalimbali.

37. Jadili faida na hasara za kuwachanganya katika darasa moja watoto wenye ulemavu na wale walio wazima kiafya.

38. Utawatumiaje wazazi na viongozi mbalimbali kuweza kupata vifaa maalumu au huduma maalumu wanayohitaji watoto wadogo wenye ulemavu mbalimbali?

39. Eleza maana na madhumuni ya Elimu ya Watu Wazima nchini Tanzania.

40. Chagua harakati tano za kuimarishaElimu ya Watu Wazima Tanzania na ueleze jinsi kila harakati ilivyotekelezwa.

41. Mwalimu J.K Nyerere alikuwa na mitazamo gani kuhusu Elimu ya Watu Wazima?

42. Eleza tofauti kati ya maneno yaliyowahi kutumika kuelezea elimu wapewayo watu wazima.

             (a). “Elimu ya ngumbaru”

             (b). “Kisomo chenye manufaa”

             (c). “Elimu ya Watu Wazima”

             (d). “Elimu/Kisomo cha Kujiendeleza”.

43. Taja na eleza sifa tano kuu za mwanafunzi mtu mzima.

44. Eleza matakwa ya mwanafunzi mtu mzima kiakili, kimaumbile, kijamii, kisaikolojia na kimazingira.

45. Taja na fafanua vifaa vitano muhimu vya kufundishia Elimu ya Watu Wazima.

46. Taja aina kuu nne za viongozi na eleza sifa za kila mojawapo wa aina hizo.

47. Taja na fafanua mambo makuu matano ambayo Mwalimu Mkuu au mwalimu yeyote Yule haruhusiwi au ni mwiko kuyafanya.

48. Uongozi wa pamoja ni nini, una faida gani kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi.

49. Pamoja na ubovu uliopo katika mtindo  wa uongozi wa kiimla, bado baadhi ya viongozi wa shule za msingi huutumia. Jadili.

50. Eleza matatizo au hasara inayoweza kusababishwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi kuwa kiongozi aliyebweteka.

51. Taja na fafanua majukumu makuu manne ya mwalimu mkuu wa shule za msingi.

52. Eleza majukumu ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi:

               (a). Kama mtawala

               (b). Kama mwendeshaji

53. Taja na fafanua majukumu kumi ya kamati ya shule.

54. Eleza jinsi mwalimu mkuu wa shule ya msingi anavyoweza kusimamia mapato na matumizi ya shuleni.

55. Ualimu ni kazi na vile vile ni taaluma. Jadili

56. Jadili aina hizi mbili za walimu kwa kuangalia faida na hasara zake:

               (a). Mwalimu mwelekezaji na mwezeshaji

               (b). Mwalimu ndiye kisima cha taaluma na ujuzi

57. Taja na fafanua sifa kuu zinazofanya ualimu uwe kazi ya kitaalamu.

58. Eleza unavyokubaliana au kukataliana na usemi kwamba “mwalimu kazi yake ni kuhamisha taaluma kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine”.

59. Kwa nini watu huibeza na kuipuuza kazi ya ualimu?

60. Eleza masharti ya kuajiriwa mwalimu asiyekuwa raia wa Tanzania.

61. Eleza masharti ya mwalimu kupandishwa daraja.

62. Eleza hatua anazotakiwa kupitia mwalimu anayeajiriwa kwa mara ya kwanza.

63. Taja madhumuni kumi ya Chama cha Walimu Tanzania, (CWT).

64. Eleza maana ya falsafa ya elimu.

65. Falsafa ya elimu ina umuhimu gani?

66. Eleza mambo makuu matano yanayojitokeza kwenye mawazo ya J.K Nyerere kuhusu elimu.

67. Ni katika masuala gani Nyerere na Sekou Toure wanalingana kuhusu elimu?

68. Linganisha mbinu za kufundishia anazohimiza Freire na zile anazohimiza Montessori.

69. Ni vipengele gani vya elimu ya awali anavyopendekeza Montessori vinatumika hapa nchini?

70. Taja na fafanua mambo makuu matano yaliyosisitizwa katika falsafa ya elimu ya Sekou Toure.

71. Eleza tofauti kati ya elimu ya awali na elimu ya msingi.

72. Kuna ubaya gani kuiita elimu ya awali “Shule za Vidudu”?

73. Eleza huduma muhimu wanazostahili kupatiwa watoto wa elimu ya awali.

74. Fafanua mbinu zinazofaa kufundisha elimu ya awali.

75. Eleza tofauti iliyopo kati ya mbinu za kufundishia elimu ya awali na elimu ya msingi.

76. Taja aina kuu za watoto wenye mahitaji maalum.

77. Unadhani ni kwa nini watoto wenye mahitaji maalum wanachanganywa na wale wa kawaida darasani?

78. Eleza jinsi utakavyowasaidia watoto wenye mahitaji maalum darasani mwako.

79. Eleza maana ya Elimu ya Watu Wazima kwa mtazamo wa Mwalimu J.K Nyerere.

80. Taja na kufafanua vipengele vitano kuthibitisha umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima kwa Watanzania.

81. Eleza jinsi serikali ilivyojitahidi kuimarisha Elimu ya Watu Wazima katika miaka ya sabini hadi themanini.

82. Eleza tofauti iliyopo kati ya mwanafunzi mtu mzima na mwanafunzi mtoto wa shule.

83. Jadili sifa tano za mwanafunzi mtu mzima.

84. Taja na eleza matakwa ya mwanafunzi mtu mzima.

85. Taja mambo ambayo huweza wanafunzi watu wazima kupenda kujifunza.

86. Eleza tofauti iliyopo kati ya utawala na uendeshaji wa shule ya msingi.

87. Eleza majukumu ya kamati ya shule ya msingi.

88. Eleza majukumu ya kamati ya taaluma ya shule ya msingi.

89. Eleza mambo matano yanayofanya kazi ya ualimu hapa Tanzania iwe ngumu.

90. Taja na fafanua haki na wajibu wa mwalimu.

91. Taja masharti matano ya ajira ya kudumu.

92. Fafanua kazi tano za Tume ya Utumishi kwa Walimu.

93. Kuna umuhimu gani kwa mwalimu kujiunga na CWT?

94. Taja na fafanua majukumu ya CWT.

95. Kuna uhusiano gani kati ya CWT na TFTU?

96. Taja masharti ya kujiunga na CWT.

97. Taja na eleza haki za wanachama kamili na shiriki katika CWT.

98. Taja na fafanua kwa ufupi mitazamo ya wanafalsafa wa elimu watano unaowafahamu.

99. Eleza tofauti iliyopo kati ya Falsafa na Sosholojia

100. Fafanua istahi zifuatazo

               (a). Haki

               (b). Wajibu

               (c). Nidhamu

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

19 thoughts on “Jipime | Maswali 100 Wikiendi hii | Misingi ya Elimu

    1. Asante Skitu nimefurahi kukuona umetembelea ukurasa huu naimani utawapa na wengine anuani yetu ili nao waje kuangalia na kupata maarifa yaliyopo, nawe karibu tena mara kwa mara. Asante

      Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.