Jipime Usiku huu na Mbinu za Kufundishia Hisabati

Mbinu za Kufundishia Hisabati
“The great thing in this world is not so much where we are, but in what direction we are moving”

1. Fafanua umuhimu wa kutumia mbinu shirikishi katika kujifunza Hisabati.

2. Kuna tofauti gani kati ya njia za kufundishia na mbinu za kufundishia Hisabati?

3. Kuzidisha ni kujumlisha kwa kurudiarudia. Thibitisha usemi huu kwa kutumia mfano huu 2 x 6.

4. Taja sababu nne zinazomfaya Mwalimu wa somo la Hisabati kutumia zana za kufundishia.

5. Eleza utakavyofundisha wanafunzi wako kugawa 12 kwa 4.

6. Bainisha tofauti zilizopo kati ya Malengo ya Jumla na Malengo Mahsusi ya somo.

7. Taja vifaa vitano vilivyoko katika mkebe wa Hisabati vinavyotumika kufundishia Jometri.

8. Utamthibitishiaje mwanafunzi wa darasa la tano kuwa 3/5 = 60%.

9. Eleza umuhimu wa vifaa vifuatavyo katika somo la Hisabati;

              (a). Kiguni

              (b). Kipimapembe

10. Utawashawishi vipi wanafunzi wa darasa la V kuwa ½ = 2/4 = 4/8 = 8/16.

11. Kwa kutumia vielelezo eleza utakavyowathibitishia wanafunzi wa darasa la saba kuwa jumla ya nyuzi za ndani za pembetatu ni 180.

12. Eleza hatua utakazozifuata kuthibitisha kwa wanafunzi wa darasa la tano kuwa 1/6 ÷ 2/3 = ¼.

13. Onesha hatua kwa hatua utakavyofundisha darasa la V kuzidisha sehemu. Tumia 2/5 x 1/3 kama mfano.

14. Utamthibitishiaje mwanafunzi wa darasa la sita kuwa Eneo la Trapeza yenye pande mbili “a” na “b” ambazo ni sambamba na kimo “h” ni ½h(a+b).

15. Andaa somo la Hisabati kufundisha darasa la sita kuhusu pembe.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

4 thoughts on “Jipime Usiku huu na Mbinu za Kufundishia Hisabati

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.