Ufundishaji wa Sayansi

Mbinu za kufundishia Sayansi
Mbinu za Kufundishia Somo la Sayansi

Walimu wengi katika shule za msingi hawapendi kufundisha somo la Sayansi. Sababu kubwa inayotolewa ni kuwa somo la Sayansi ni gumu kufundisha na kwamba linahitaji vifaa vingi vya kufundishia ili lifanikiwe.

Kwa misingi hii walimu wengi wanapofundisha Sayansi huwapa wanafunzi kitabu cha kiada na kuwataka wanafunzi wavisome kwa sauti au kimya.

Matokeo ya ufundishaji huo wa Sayansi huwafanya wanafunzi walichukie somo la Sayansi shuleni na baada ya kumaliza shule.

Hivi sasa kila shule ya msingi ina dhamana na jukumu la kuimarisha na kuboresha ufundishaji wa Sayansi.

Enzi ya leo ni enzi ya Sayansi na Teknolojia na mabadiliko mengi yanatokea kwa kasi sana. Kufundisha na kujifunza Sayansi hakuna budi kufanyika.

Kuendana na mabadiliko haya, Sayansi inayofundishwa katika shule za msingi ni ile itakayomwezesha mwanafunzi kuchunguza mazingira yake kisayansi, kuwa katika hali ya usalama yeye na jamii nzima na kuweza kuelewa kisayansi matukio mbalimbali yanayotokea.

Katika uwanda huu ungana hapa hapa na Mwalimu Gunda kupitia barua pepe jiandaetz@gmail.com ili kuwezesha jinsi gani ufundishaji wa Sayansi katika shule za msingi unavyoweza kukuzwa na kuboreshwa ili uwe na manufaa katika maisha ya wanafunzi.

Unakaribishwa kuchangia bila kikomo namna tutakavyoweza kueleza kwa ufasaha mbinu na njia zinazotumika katika ufundishaji wa sayansi, namna ya kukabili matatizo yanayokabili ufundishaji wa sayansi, utengenezaji na matumizi ya vifaa na zana za kufundishia zinazotokana na mazingira na namna ya kupima maendeleo ya kujifunza kwa wanafunzi.

Sisi sote tuna jukumu la kuungana na kuimarisha juhudi na nguvu za pamoja ili kuinua vipaji vya watoto wetu kwa kuwasaidia kuwa wabunifu zaidi. Kama mwalimu unajukumu la kuona umuhimu wa maisha ya baadae ya mwanafunzi wako mbali na hali ngumu iliyopo kimaslahi na ufundishaji tunahitaji kuwa wazalendo pale unapoona inafaa kuwa; na sasa inafaa kuwa hivyo.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

5 thoughts on “Ufundishaji wa Sayansi

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.