Mbinu za Kufundishia Sayansi | Ushirikishwaji wa Mwanafunzi katika Kufundisha Sayansi.

Tunapofundisha wanafunzi somo la Sayansi tunataka wapate stadi na maarifa mbalimbali kuhusu vitu vinavyowazunguka. Ili wanafunzi waweze kufurahia somo hili na kupata stadi hizo zinazohusiana na Sayansi, itabidi mwalimu atumie mbinu za kufundishia zinazo mmotisha mwanafunzi. Mwanafunzi atakuwa mtendaji mkuu ikiwa atashughulishwa katika harakati za kujifunza.

Mbinu ya Maswali

Sayansi ni mojawapo ya masomo ambayo yanaweza kufundishwa kwa ufanisi kwa kutumia Maswali. Katika njia hii mwalimu anawauliza wanafunzi maswali na wanafunzi hutoa majibu. Kwa kawaida, mwalimu anauliza wanafunzi swali ambalo lina jibu sahihi moja tu na jibu hilo kwa kawaida ni fupi; neno moja tu.

MBinu za Kufundishia Sayansi
Mbinu ya Maswali na Majibu

Ikiwa mwanafunzi anatoa jibu sahihi anatakiwa kupongezwa kwa maneno kama “vizuri” au “sawa”. Kama mwanafunzi anatoa jibu ambalo si sahihi basi mwalimu alikatae kwa njia nzuri kama vile kusema “Si sahihi sana” au “Nani mwingine ajaribu”.

Kutokana na jibu sahihi la mwanafunzi, mwalimu anatunga swali lingine na hivyo kuendelea mpaka anafika lengo la somo lake.

Tuchukue mfano wa mwalimu anayefundisha sifa na sehemu za insekta, “panzi”.

Mwalimu: mnamuona insekta huyu?

Wanafunzi: Ndiyo

Mwalimu: anaitwaje?

Mwanafunzi 1: Panzi

Mwalimu: vizuri, hivyo vitu viwili kichwani vinaitwa nini?

Mwanafunzi 2: vinaitwa pembe

Mwalimu: hapana, sio pembe nani mwingine ajaribu

Mwanafunzi 3: vinaitwa papasi

Mwalimu: vizuri, unafikiri kazi ya papasi ni nini?

Mwanafunzi 4: kuonea

Mwalimu: unataka kusema hayo ni macho?

Mwanafunzi 5: Hapana, kazi ya papasi ni kupapasia

Mwalimu: sawa, je insekta huyu ana mabawa mangapi?

Mwanafunzi 6: manne

Mwalimu: vizuri, ana miguu mingapi?

Mwanafunzi 7:  miguu sita

Mwalimu: sawa kabisa, ungeambiwa ugawanye mwili wa insekta huyu katika sehemu kuu, ungepata sehemu ngapi?

Mwanafunzi 8: sehemu kuu tatu

Mwalimu: sehemu hizo ni zipi?

Mwanafunzi 9: kichwa, kifua na tumbo

Mwalimu: Vizuri sana, Taja wadudu wengine walioko katika kundi la insekta

Mwanafunzi 10: nzige, nyuki, inzi n.k.

Manufaa ya njia hii.

  1. Njia hii inawashirikisha wananfunzi katika tendo la kujifunza
  2. Hufundisha wanafunzi stadi za kuchunguza na kujenga uwezo wa mwanafunzi wa kufikiri ili kujiongezea maarifa, kujenga mambo juu ya uzoefu wa mwanafunzi;
  3. Hupunguza kutumia njia ya mhadhara peke yake

Mapungufu ya mbinu hii

  1. Wanafunzi hawana budi kuwa na uzoefu wa mada/kipengele kinachofundishwa;
  2. Mwalimu lazima ajue namna ya kurekebisha au kugeuza swali ili apate jibu analotazamia;
  3. Mwalimu awape wanafunzi moyo wa kupenda kujieleza na kutoa mawazo yao kwa uhuru;
  4. Hakuna uhakika kuwa wanafunzi wote katika darasa zima wanafuata mafundisho ya mwalimu.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Mbinu za Kufundishia Sayansi | Ushirikishwaji wa Mwanafunzi katika Kufundisha Sayansi.

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.