Tufiche uchumba wetu, Tutangaze yetu ndoa!

Mateno Ramadhani
Mateno Ramadhani na Yakuti

Bismilahi awali,Nijina lake manani,
niweze kutanabali,Yaliyo mwangu kinywani,
Kwa uwezo wa Jalali,Ya kheri kuyabaini,
Ya Raufu tujaliye,Tufikia nusu dini.

Mwezi nne ilikuwa,Elfu mbili na saba,
Uchumba ukawadia,Kwa hekima za swahaba,
Mtume hakubakia,Alifundisha ya shaba,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Tufiche uchumba wetu,Tutangaze yetu ndoa,
Tutayakwepa ya watu,Rasuli kashuhudia,
Siyo kwamba ni watu,Vitabu kuelezea,
Ya Raufu tujaliye,kufikia nusu dini.

Siku nyingi uliwaza,Kumpata mke mwema,
Sala suna uliweza,na kufunga kwa hekima,
kakuwezesha Muweza,Kuchagua kwa salama,
Ya Raufu tujaliye,kufikia nusu dini.

Mwezi wa nane mapema,Nane elfu mbili,
Ilipitika khekima,Uchumba kuubashili,
Tulijifunga mitima,Nakuonesha kujali,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Tunakuomba Manani,Afya njema utujali,
Subira utujalini,Uvumilivu asili,
Nifike kwake chumbani,Nimtoe udhalili,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Tuoane kwa kujenga,Isiwe ni kujaribu,
Msingi ni kuujenga,Kwa upendo kuratibu,
Naamini tutajenga,Tukiweka ukaribu,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Mpenzi nasikitika,Kuitamka kwakheri,
Mwezi tisa ikifika,Safari nitaijili,
Kuaga nalazimika,Nakuombea la kheri,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Si kwamba nafurihia,Machozi yananitoka,
Nini ninakuachia,Furaha ikakufika,
Mapambo ningeachia,Amani ikakufika,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Naomba unielewe,Niko kando pembeni,
Mawazo uyaondowe,Niendako ni nyumbani,
Unakaribishwa nawe,Uingiye safarini,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Ninaomba kuusia,Nafsi yangu na yako,
Dunia ya angamia,Kwa kukiuka andiko,
Starehe inaua,Hii kweli ni tamko,
Ya Raufu tujaliye,Kufikia nusu dini.

Kumi mbili nasimama,kaditama naeleza,
Lengo langu nalisema,Ingawa laniumuza,
Kwakheri ninaisema,Anayejua Muweza,
YARAUFU tujaliye,Kufikia nusu dini,

© Mateno Ramadhani Shairi kutoka kwa YAKUTI (“HANI……………” )27. 08. 2008

 

mateno na bakaza
Mateno na Bakaza

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Tufiche uchumba wetu, Tutangaze yetu ndoa!

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.