TUME YA MH PINDA IMETOA MAPENDEKEZO 130

Sema ukweli hata kama unauma

Jumla ya mapendekezo 130 yametolewa na tume ya Kuchunguza Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012. Mojawapo ni kupitiwa upya kwa mitaala ya elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vya ualimu.

Hayo yamethibitishwa na mwenyekiti wa tume hiyo Prof Sifuni Mchome. Prof Mchome alisema mitaala iliyopo imeshapitisha muda wake kwani kwa kawaida mtalaa unabadilishwa baada ya kumaliza mzunguko wake mmoja, hivyo tume hiyo imependekeza kupitiwa upya kwa mitaala yote ambayo imemaliza mzunguko. Mzunguko huu ni miaka saba kwa elimu ya msingi, minne kwa sekondari na miwili kwa kidato cha tano na sita.

Pendekezo la kubadili mtaala maana yake nini?
Kama mitaala iliyopo ilishamaliza mizunguko yake siku nyingi bila kufanyiwa mabadiriko stahiki, maana yake mitaala iliyopo haiendani na hali halisi ya sasa. Kwa bahati mbaya sana, elimu isiyoendana na hali halisi katika jamii-inakuwa haina mvuto kwa wanafunzi kujifunza. Hawaoni kuhitaji kutumia maarifa wanayojifunza katika maisha yao moja kwa moja. Kukosa mvuto pia kunadumaza nia ya wanafunzi kuwa wadadisi na wabunifu. Kama ilivyowahi kuelezwa na wadau wengi miaka ya nyuma, tunapokosa mtaala unaoendana na hali yalisi ya sasa ni kwamba tunawaumiza wanafunzi na kuharibu misingi ya elimu tuliyoirithi.

Prof Mchome aliongeza: “…Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005 umetekelezwa bila kufanyiwa majaribio (piloting).”

TAFAKARI!

©HakiElimu

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

2 thoughts on “TUME YA MH PINDA IMETOA MAPENDEKEZO 130

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.