KIJIWENI WAJADILI VURUGU MTWARA

Imeandikwa na Nyanda Josiah Shuli
Imeandikwa na Nyanda Josiah Shuli

Nimepita kijiweni kwangu nikakuta ‘wana’ wanabishana kuhusu machafuko Mtwara. Mmoja akasema: “Wale jamaa wanakurupuka tu. Ngoja hao waliokamatwa waonje joto ya jiwe…Hapa bongo, ukishapata matatizo tu…kila aliyekupambanisha anakukana…” Mwingine naye akadakia: “Poa tu kama vipi…maisha yenyewe magumu, angalia mwili mkubwa (anamzodoa mwenzie) halafu unasubiri ufe kwa malaria..si ni heri ukafe kwenye mapambano, ieleweke kuwa kuna haki ulikuwa unaidai ila ukanyimwa?” Mwingine wa tatu naye akatupia ya kwake: “Hizo ajira wanazozitaka huko ni za aina gani? Hao jamaa wamesoma? Wanaweza kuishia kuchimba mitaro tu na kubeba vitu vizito begani…kazi nzuri mpaka uwe umeenda shule mwanangu…sisi ambao hatukusoma tutaishia kuosha magari ya wasomi tu, hata kazi zikiwepo zitaenda kwa wengine tu…” Poleni kwa kuwachosha; ila nimalizie na mwingine ambaye naye alikandamiza: “Kwani bongo kuna shule? Kama ipo mbona wamefeli nchi nzima?” hapa tunayeyushana tu…hakuna mchongo wala nini. Sanasana Mjomba ana lake jambo. Anataka kila kitu kihamie Bagamoyo..”

Mjadala ule uliendelea mpaka nikaondoka. Nikitafakari majibizano hayo ya ‘wana’ naona kuna mpasuko wa tafsiri wa kile kinachoendelea huko Mtwara. Kumbe hata ubabe tu hauwezi kumaliza tatizo kwa sababu kuna kundi kubwa la watu hawana cha kupoteza, hata ikiwa ni kufa-poa tu. Je kuahirisha kujadili masuala ya nishati na madini itasaidia? La hasha.

Hatua za makusudi zinahitajika-hasa kuanza upya kwa mkakati wa mjadala wa umma kuhusu suala zima la gesi hiyo. Mjadala ujikite katika mambo haya:

1) Gesi ya asili ni nini hasa?

2)Inaweza kuvunwaje?

3) Watanzania watanufaikaje?

4) Wanamtwara-na Lindi nao watafaidikaje?

5) Kuna uwekezaji gani utafanyika Mtwara na lini?

6) Kwa nini ni muhimu gesi isafirishwe?

7)Fursa zipi wazawa wanaweza kuchangamkia?

8) Hata wale wasioojua la kufanya-wawezeshweje ili wasipitwe na maendeleo ya Mtwara?

Haya ni baadhi tu ya mambo ya kujadiliwa ili tuondoe hali ya kutokuaminiana. Hivi sasa-kila anayewapinga wananchi wa Mtwara anaonekana machoni kwao ni adui. Hawatamdhuru tu endapo hawana namna ya kumfikia, Hawa jamaa zetu-hawaelewi somo. Wanaweza kutulia-halafu wakashambulia kwa kushtukiza (msisahau kuwa wana asili na vita vya maji-maji).

Binafsi nasikitishwa sana na vurugu hizi. Hata hivyo umakini wa hali ya juu unatakiwa katika kukabiliana na tatizo hili. Serikali ikijikanyaga na kuanza kutoa ahadi hewa-itakuwa imejitengenezea mazingira magumu-kiasi kwamba watanzania wengine wanaoishi ziliko raslimali nyingine nao wataanza kudai kama walivyopewa wana wa KUSINI. Tanzania ni moja, na kila mmoja ni ndugu na mlinzi wa mwenziye; ndivyo TANU ilivyotufundisha.

©Nyanda Shuli

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.