Wapi CCM imekuwa na BUSARA kutumia RASILIMALI za nchi hiii?

©Stanslaus Nyembea

Sema ukweli hata kama unauma
Sema ukweli hata kama unauma

Nimejaribu kuelimisha kiutaalamu madai ya msingi ya wanamtwara. Wako sahihi kwa 100%. Nchi zenye akili, sio inayoongozwa na CCM, rasilimali,huwa kwa kiwango fulani, zinabaki sehemu zinakozalishwa/toka.

Mfano, wanyamapori, jamii za jirani hupata mgawo wa 25% ya mapato ya uvunaji. Kwa nchi zenye akili, Australia, New zealand na zinginezo, kwenye gesi na mafuta ya ndani ya eneo la bahari (3 nautical miles) gasi na mafuta ni ya jimbo husika. Kwenye bahari kuu, offshore, mapato yanagawanwa kati ya serikali na watu wa eneo husika kwa makubaliano maalumu, MOU.

Kwa kesi ya Mtwara, pia, ilitakiwa iwe hivi. Ubovu wa serikali dhalimu ya CCM, uonevu na wizi wa rasilimali waliouzoea kwenye madini, tembo, ndege za nchi, reli, bandari n.k wanakataa ukweli huu.

I wapi dhambi ya kudai manufaa kwenye gesi inayotoka eneo lao? Kwanini kenye wanyama haki hii ipo? Kuna watu wanadai serikali ilitumia fedha kutafiti gesi- Hawa ni Mambulula hayajui eneo hili la gesi .

Kwa usahihi utafiti wa gasi na mafuta hufanywa na kampuni husika kwa makubaliano ya kugawana ges na mafuta vikipatikana/mapato-production sharing agreements husainiwa. Kazi ya serikali ni kuandaa VITALU vya utafiti tu, kisha wanohitaji wanaomba na kupatiwa.

Huu ndiyo ukweli na usahihi wa jambo hili. Gasi lazima iwafae kwanza wanamtwara, mathalani 15-25% ya mauzo ya gesi yote ibaki Mtwara-kisha nchi yote inufaike pia. Ahadi za Viwanda ni upuuzi wa CCM na umbumbu wa kila siku.

Kiwanda gani cha serikali kipo HAI nchi hii cha kutoa ajira, mbolea Minjungu kipo mahututi, Urafiki kipo wapi ubungo, mwatex mwanza?? CCM, acheni ujinga, tumieni akili si nguvu kila mahali.

Hakuna mkono wa siasa, kutaka umaarufu wala ndumba.

Hamna aibu kwa wizi mlioufanya kwa miaka mingi kuhusu rasilimali za nchi hii!!!.

Wapi CCM imekuwa na BUSARA kutumia RASILIMALI za nchi hiii????? Wapi CCM imekiri kukosea na kujisahihisha?????

NAWASILISHA.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Wapi CCM imekuwa na BUSARA kutumia RASILIMALI za nchi hiii?

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.