Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama amempongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete

1016403_493003840769003_1185048653_n
Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama amempongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutoa elimu bure kwa watoto Wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi .

Mama Obama alizitoa pongezi hizo leo wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.

“Jana nilitembelea makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto ambao baadhi yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya”, alisema Mama Obama.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika
ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya, elimu na ujasiriamali.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.

Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara la Afrika.

Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.

Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika Afrika.
— in Dar es Salaam.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.