FAHAMU VIPAUMBELE VYA MATOKEO MAKUBWA SASA KATIKA ELIMU (BIG RESULTS NOW)

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Elimu) ulizinduliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo jana na kutaja mikakati 9 ifuatayo: Hebu pitia mikakati hii-kisha utoe maoni yako kama inajitosheleza.

corruption

1. Upangaji wa shule kwa ubora wa matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule iliyoongoza hadi ya mwisho. Lengo la mkakati huu ni kuongeza uwajibikaji na ushiriki wa jamii katika usimamizi wa utoaji wa elimu bora.

2. Utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora zaidi.

3. Kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule. Mkakati huu utasaidia kuimarisha utendaji wa shule kwa kuwawezesha viongozi wa shule kutekeleza majukumu yao kikamilifu

4. Upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu. Lengo la mkakati huu ni kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu katika madarasa ya chini ya elimu ya msingi kabla ya kujiunga na madarasa yanayofuata

5. Utoaji mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi za KKK. Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha walimu kumudu ufundishaji wa stadi za KKK katika darasa la kwanza na la pili. Mafunzo yatatolewa kwa walimu kutoka shule 6,167 za halmashauri 40.

6. Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na kujifunza-Students Teachers Enrichment Program (STEP). Mkakati huu utajenga utamaduni wa kuwabaini wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika kujifunza. Aidha, utoaji mafunzo ya walimu kwa ajili ya utekelezaji yanalenga kumpa mwalimu nyenzo na uwezo zaidi wa kufundisha na kubaini na kuzingatia maeneo yenye changamoto kwa wanafunzi.

7. Ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule. Lengo la mkakati huu ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa vifaa muhimu shuleni.

8. Utoaji ruzuku ya uendeshaji wa shule. Utekelezaji wa mkakati huu utawezesha uboreshaji wa upatikanaji vitabu vya kiada na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.

9. Utoaji wa motisha kwa walimu. Mkakati huu utawezesha kuwatambua walimu, kutatua changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha za kifedha na zisizo za kifedha kwa kujali maslahi na madai yao ya kimsingi.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

11 thoughts on “FAHAMU VIPAUMBELE VYA MATOKEO MAKUBWA SASA KATIKA ELIMU (BIG RESULTS NOW)

 1. Mikakati hiyo ni mizuri! Ila serikali iboreshe mazingira ya kufundishia yatakayo wapa morali WALIMU wa kufanya kazi PIA walipe MADENI ya walimu na kuboresha na kutoa MISHAHARA kwa wakati Hapo ndipo mpango wa Biglisult Now UTAWEZA KUFANIKIWA

  Like

 2. Mpango wa matokeo makubwa sasa katika Elimu ni ndoto za mchana kama serkali haitawajali walimu katika maslahi hasa katika kuwalipa mishahara inayoridhisha ,fikiria mbunge anayekaa bungeni kwa muda wa miezi mitatu na kila asubuhi anapokea bahasha ya posho ya kila siku kando ya mshahara wa milioni kumi na mbili kwa mwezi wakati mwalimu anakaa shuleni kwa siku thelathini akifuta makamasi ya kuwapeleka watoto chooni anapata laki tatu hadi nane wakiwepo na watoto wa mbunge.Kwa hali ilivyo tusitegemee Bigresult bali tutegemee Poor result

  Like

  1. Ni kweli kabisa kaka.Tena serikali hisipotengeneza mazingira mazuri na mishahara & posho zinazoendana na gharama ya maisha ya sasa na baadae basi isitegemee kupata matunda mazuri ktk mpango wao wa MATOKEO MAKUBWA SASA

   Milto@———- Sent from my Nokia Phone

   Like

 3. KWELI KAMA SERIKALI INAMPANGO HUO NI VUZURI KWA AJILI YA kuinua kiwango cha elimu, ila inajukumu la kuboresha mazingira YA MWALIMU MAANA YEYE NDIE MWEZESHAJI HAPO NDIPO MALENGO HAYO YATAFIKIWA¸

  Like

 4. Serikali inastaili pongezi kwa kiasi cha malengo kilichofikiwa lakini pia upande mwingine inasababisha kutofikiwa malengo mahususi kwa sababu mbalimbali kama zifuatazo 1.motisha kwa walimu na wanafunzi wanapofanya vizuri 2.mazingira ya kufanyia kazi hayakizi kiafya 3.shule nyingi zina mabara isiyokamili na zingine hazina kabisa,4.walimu washirikishwe kupanga mikakati ya Matokeo makubwa sasa.5.mwl.apatiwe mafunzo kazini ili kumpanua akili.

  Like

 5. Big result inaweza kuwa na matunda mazuri endapo kauli ya mh.rais ya kuongeza mshahara na kupunguza kodi itatekelezwa hii aliitoa jijini dar.ktk sherehe za mei mosi hivyo basi wafanyakazi nao kwa ujumla kila mmoja awajibike kwa nafasi yake ili kufanikisha malengo ya serikali yetu.

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.