Tunawashukuru READ International Kwa Msaada wenu wa Vitabu

BOX 35 zilikabidhiwa leo kwa Mwalimu Gunda kwa ajili ya Maktaba ya Jamii Kabanga
Jumla ya BOX 35 zilikabidhiwa na Montse Penjuan Country Director Tanzania wa Shirika la  Read International  leo kwa Mwalimu Gunda kwa ajili ya Maktaba ya Jamii Kabanga

Tunapenda kuwashukuru shirika la READ International kwa msaada wao wa Vitabu Box 35 walizozikabidhi leo tarehe 10/10/2013 kwa Mwalimu Gunda kwa ajili ya Maktaba ya Jamii kabanga.

Vitabu hivyo vipo vya ngazi tofauti tofauti kuanzia elimu ya Chekechea hadi Chuo Kikuu. Kila mtu anakaribishwa kutembelea Maktaba ya Jamii Kabanga na Kujionea na Kujisomea Vitabu hivi pia unaweza kuazimwa kama ni mwenyeji wa Kabanga au Kasulu.

Kwa sasa utaratibu unafanyika ili kuweza kuvisafirisha hadi Kigoma Wilayani kasulu katika Kijiji cha kabanga, ukiwa kama mdau unaweza kuchangia na msaada wako unahitajika sana ili tuweze kuvisafirisha vitabu hivi, kwa kiasi chochote utakachojaaliwa unaweza kutuchangia na Mungu akikujaalia unaweza kutusaidia gharama zote za usafiri.

Kwa wale wadau wa Elimu watakaopenda kuchangia au ambaye yuko tayari kutusaidia gharama za usafiri awasiliane na Mwalimu Gunda kwa namba hizi; +255 786 92 62 85 (Airtel), + 255 767 92 92 96 (Voda) na + 255 714 22 78 75 ( Tigo).

Kwa Pamoja tunaweza kuleta mabadiliko katika Elimu kwa manufaa ya watoto wetu na jamii zetu.

Mwalimu Gunda

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.