Falsafa ya Elimu ya Awali

Ni nini Chimbuko la neno falsafa?

Neno Falsafa  hutokana na maneno mawili ya kiyunani yaani philo lenye maana ya upendo na Sophia linalomaanisha hekima.  Hivyo utaona kuwa falsafa ni Taaluma inayojishughulisha katika kutafuta ukweli wa jambo kwa njia ya kutafakari.

MBinu za Kufundishia Sayansi
Falsafa ya Elimu ya Awali

Na falsafa ya elimu ni nini? 

Ni tawi la falsafa yaani fikra za kifalsafa zilizoelekezwa kwenye masuala ya elimu.  Katika falsafa hutolewa mwelekeo unaozaamalengo makuu na malengo mahsusi, hutazama pia nafasi ya mwalimu na mwanafunzi katika masuala ya kielimu.

Falsafa ya elimu ya awali ni nini?

Ni nadharia na falsafa za elimu ambazo zimesaidia kutoa mwanga wa malengo katika Mtaala wa Elimu ya Awali, mbinu za kufundishia, utengenezaji na ufaragui wa zana za kufundishia mtoto yenye kujikita katika elimu ya awali.

Kupitia falsafa ya elimu ya awali watu huweza kuanzaisha kuendesha na kuendeleza utoaji wa elimu hiyo kwa kutumia misingi inayokubalika na jamii katika nchi nyingi.

Kwa ujumla falsafa ya elimu ya awali inatumika katika mawanda mapana ya kielimu ukizingatia kwamba ni tawi la kwanza kabisa lenye kuizungumzia kwa kina elimu katika ngazi ya awali na kuwezesha kupata mitazamo mbalimbali ya watu mbalimbali kutoka kila kona ya ulimwengu.  Michango mbalimbali ya falsafa ya elimu ya awali zimesaidia katika:

 • Kuanzisha na kuendeleza elimu ya awali
 • Kuonesha njia kwa kubuni mipango ya elimu ya muda mrefu na mfupi kuhusu elimu ya awali.
 • Kuonesha falsafa ya elimu ya kujitegemea Tanzania.
 • Kusaidia kujenga utu na maadili mema kwa walimu na wanafunzi wa E/Awali
 • Kufafanua shabaha za elimu na jinsi ya kuitoa kwa watoto wa elimu ya awali.
 • Huchambua misingi ya njia na mbinu za kufundishia na kujifunzia elimu ya awali.
 • Kufafanua wajibu na majukumu ya viongozi katika elimu ya awali.
 • Hutoa msisitizo kuhusu masomo ambayo watoto wa darasa la elimu ya awali wanapaswa kuyasoma.

Kwa ujumla falsafa ya elimu ya awali humwezesha mwalimu kufundisha vizuri na kushauri wanafunzi ipasavyo wakiwa darasani, kazi za nje hata kwenye matukio ya kimichezo halikadhalika anapokuwa anaandaa zana za kufundishia, kuwaongoza darasani hata kuwarekebisha watoto inakuwa ni kwa manufaa pindi unaptoumia nadharia za wana falsafa wa elimu ya awali.

Michango ya wanafalsafa katika elimu ya awali

Katika mada iliyopita umejaribu kujifunza mambo kadhaa yenye kukueleza hasa umuhimu wa falsafa ya elimu ya awali.  Umeona jinsi gani falsafa hii ilivyokuwa ndiyo chimbuko la msomi wa baadaye kwani mtoto wa shule ya awali leo ndiyo profesa hapo kesho katika mada hii tutajadili kwa upeo wa kutosha hata utaweza kupata kuwaelewa vema wanafalsafa na kile walichochagua kwenye elimu hii ya awali.

Wanaelimu mbalimbali walitoa falsafa zao katika nyakati tofauti kwa malengo tofauti.  Aidha wewe kama mdau wa elimu kwa sasa unatakiwa kuzijua nadharia na falsafa za elimu ya awali ambazo zimesaidia kutoa mwongozo wa kutosha katika kumfundisha mtoto mdoto.

Inaaminika kuwa kwa kuzitumia nadharia na falsafa hizo, pamoja na kuzifasili unaweza kueleza maana ya nadharia, kuchambua nadharia na falsafa za kielimu na tena kuzitumia kuiendeleza elimu ya awali.

Mbali na hayo falsafa za wataalamu wengi zimeweza kusaidia sana katika kuanzisha na kuendeleza elimu ya awali, kutekeleza majukumu ya uendeshaji wa shule ya awali, kupima maendeleo ya elimu ya awali, kusimamia ubora wa elimu ya awali hata kupambana na changamoto za uendeshaji.

Baadhi ya wana falsafa mbalimbali na namna walivyochangia uwepo wa elimu ya awali kama ifuatavyo:

i) John Dewey (1859-1952)

Ni mmarekani aliyeanzisha kituocha watoto alichokiita Maabara (1886) kwa ajili ya kufanya majaribio juu ya namna ya kujifunza kwa watoto miaka (4-13) aliamini kuwa katika kutenda mtoto hujifunza zaidi na kupata maarifa.  Yeye alitaja mambo muhimu ya kumfundisha mtoto kama vile:

 • Watoto watumie mazingira halisi
 • Watoto wajifunze kwa ktatua tatizo la kweli na lichochee ari ya kujifunza.
 • Mtoto apewe muda wa kufanya jaribio
 • Mtoto afanye uchunguzi wa kutatua.

ii)   Jean Peaget

Huyu ni mwanzilishi wa nadharia ya utambuzi na aligawa ukuzi wa watoto katika vipindi vikuu vinne (4) na kila kipindi kina maana katika kujifunza.  Kipindi cha miaka (3-6) mtoto hujifunza kwa kutumia vitu halisi.  Alisema kuwa mafunzo yalenge kumfanya mtoto aweze:

 • Kuona
 • Kuhusianisha
 • Kubuni
 • Kuumba
 • Kuunda
 • Kutumia mazingira
 • Kushughulikia akili ili ajenge maana katika ubongo

Mtoto anapojifunza jambo hutafakari kwa kuhusianisha miundo hiyo na iliyopo ubongnoi mwake.

iii) Maria Montessori

Ni mwanafalsafa wa Kiitaly mwanamke wa kwanza kuwa Daktari wa magonjwa ya watoto na ya akili aliyegundua tatizo la kuvia akili kwa watoto ni la kielimu sio tiba pekee na kwamba alivimilika.

 • Watoto hujifunza kwa ufanisi iwapo watafanya kwa vitendo
 • Mwalimu aandae mazingira mazuri ya kujifunzia
 • Mtoto ajifunze vizuri atumie michezo
 • Mtoto apewe nafasi ya kuchunguza mazingira yake demokrasia.
 • Mtoto apewe uchaguzi wa mambo ya kujifunza
 • Mwalimu atumie zana zenye mvuto kwa watoto zikuze udadisi (utendaji)
 • Mafunzo yazingatie ukuzaji wa mtoto
 • Elimu ioanze napozaliwa mtoto hadi miaka 6, ili kujenga haiba.
 • Elimu ikuze mtoto kiakili, kimaono, kiroho na apate lishe bora.

iv) Lev Vygotsky

Huyu ni mwanafalsafa wa elimu aliyeamini kuwa mtoto ana uwezo wa kujifunza mwenyewe bila msaada lakini akipata msaada uwezo huo utaongezeka mara dufu.  Mwongozo aweze kutumia mbinu shirikishi kwa mtoto katika mchakato wa kujifunza.

v) Johan Henrich Pestalozzi (1746 – 1827)

Huyu ni mwanaelimu wa Kiswisi aliyotoa mchango mkubwa kwa elimu ya watoto wadogo kwani aliamini:

 • elimu iwe katika maendeleo ya mtoto.
 • elimu ishinikize maadili na maumbile na ukuzi wa akili
 • kuanzisha taasisi ya kuwapo mafunzo walimu
 • moto hujifunza kuptiia mfumo wa fahamu.
 • alianzisha shule ya watoto wadogo katika bustani yake kusaidia wazazi maskizi.

vi)  Julius K. Nyerere (1922-1999)

Mwanaelimu wa kitanzania aliyeridhia agizo la haki za watoto na kutangaza mwaka 1979 kuwa mwaka wa mtoto wa kimataifa.  Naye alikazia sana haki ya misingi kwa mtoto ambayo ni elimu, hivyo alisisitiza elimu ya watoto wadogo alimaini kuwa:

 • kuzaa ni rahisi kuliko kulea
 • wananchi lazima wajifunze umuhimu wa kulea vizuri watoto ili kupata taifa elekevu.
 • Aliweka msisitizo wa vyakula mbalimbali wakati wa ujauzito.  Kipindi cha mama kuonyonyesha na wakati wa kuachisha mtoto ziwa.
 • Elimu iwe kwa manufaa ya mtoto na jamii kwa ujumla.

vii)             Naom choamky

 • Alitafiti ukuaji wa lugha kwa mtoto
 • Ukuaji wa lugha unatokana na ubongo wa mtu
  • Alioamini kuwa kama ubongo hauna matatizo mtoto ataweza kujifunza lugha ktuoka katika mazingira yake.
  • Mtoto huzidi kupata msamiati kwa kusikia, kuongea kwa kurudia rudia kusoma na kuandika.
  • Watoto walihimizwa kuzingumza na kusoma maneno kamili.
  • Mwalimu wa elimu ya awali ajitahidi kutumia masali yatakayochochea mtoto kuongea zaidi.

viii)      Friedrich Froebel (1782 – 1858)

Huyu ni mwanaelimu wa Kijerumani aliyeanzisha shule ya chekechea ili kuwapa elimu watoto wadogo mwaka 1827.  Pia shule za awali hizo alizopa jina la shule za chekechea na aliamini:

 • Msukumo wa kujifunza hutoka ndani ya mtoto mwenyewe
 • Lazima mzazi amlinde mtoto katika kazi zake.
 • Mtoto hujifunza kwa matendo
 • Watoto wafundishwe kwa kuwafundisha.
 • Mkazo juu ya uanzishaji wa shule za watoto wadogo (chekechea na awali)

ix)                Paul Freire (1977) na Ausbel (1978)

 • Wanasisitiza matumizi ya maarifa ya awali ya mtoto
 • Ujifunzaji wenye kujenga maana (meaningful learning) huja kwa kushirikisha watoto kwenye shughuli mbalimbali.
 • Wapinga kuwa sii kweli kuwa watoto wanazaliwa wakiwa hawana kitu chochote kichwani, hivyo wanahitaji kujazwa nadharia za maarifa na walimu darasani.
 • Wanaamini kuwa watoto wanakiasi cha maarifa, stadi, na mielekeo hata kabla ya kujifunza mada yoote.
 • Wanaamini kuwa kama maarifa ya awali ya mtoto hayatatumika inaweza kuleta migogo na maarifa mapya hivyo kufanya tendo la kujifunza kuwa gumu.

Mpaka hapa umekwisha kuona mawazo ya wanafalsafa kadhaa ambao walionesha mambo ya kuzingatia kutokana na mawazo yao kuwa lengo la kumsaidia mtoto kuweza kujifunza na kuendelea shughuli za elimu ya awali ambazo kimsingi hutekelezwa karibu ulimwengu mzima.  Wana elimu wengi walionesha umuhimu wa mazingira, vifaa, mbinu shirikishi majaribio na michezo kuwa ni muhimu katika kuwafanya watoto wa shule ya awali kujifunza vizuri.

wanafunzi

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

31 thoughts on “Falsafa ya Elimu ya Awali

  1. Asante kwa Elimu mnayotupatia,,kwangu imekuwa msaada mkubwa katika masomo yangu,,,naomba kujua zaidi juu ya mwanafalsafa huyu’John Amos Comenius ‘asante

   Like

 1. Nimewapitia wanafalsa hao wote na njia au nia yao kubwa ni kuona elimu inatolewa kwa kufuata misingi walioiainisha,0744454201

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.