Jipime na Msawali 50 Kusherehekea Muhula Mpya 2014 | Maswali Mchanganyiko

 1. Mbinu za kufundishia ni nini?
 2. Elimu ya awali ni nini?
 3. Eleza umuhimu na mapungufu ya Mtaala wa elimu Tanzania.
 4. Bainisha misingi ya kufanya upimaji wa kielimu
 5. Bainisha misingi ya kufanya tathmini ya mtaala
 6. Dhana ya lugha hujipambanua katika sura kuu tano. Taja sura kuu nne za lugha.
 7. Utajuaje kuwa tendo la kujifunza limekamilika kwa mwanafunzi wako?
 8. Kuna aina ngapi za unasihi?
 9. Taja stadi za kimaadili ambazo mwalimu huzijumuisha katika upimaji wa elimu.
 10. Je, kuna umuhimu gani wa mpango wa elimu hapa Tanzania?
 11. Onesha utaratibu wa uendeshaji wa elimu nchini Tanzania kwa mujibu wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 1995.
 12. Je, umewahi kuuona mtaala wa shule ya msingi? Kama siyo kuna dosari gani ya kutouona mtaala huo?
 13. Tofautisha kati ya Utawala na Uongozi.
 14. Kwa kutumia mchoro onesha mtiririko wa Muundo wa uongozi chuoni.
 15. Nini maana ya Elimu ya watu wazima?
 16. TEHAMA ni nini?
 17. Fafanua dhana ya kusoma na kuandika.
 18. Eleza kwa kifupi maana ya Kisomo Chenye Manufaa (KCM) na Kisomo cha Kujiendeleza (KCK).
 19. Mwanafunzi mtu mzima ni nani?
 20. Fafanua dhana ya Elimu.
 21. Kujifunza kwenye maana kuna maana gani?
 22. Kwa kutumia mifano mitatu eleza maana ya kujifunza kipurure.
 23. Eleza kwa maneno yako mwenyewe maana ya “Uhawilishaji wa Maarifa”.
 24. Eleza kwa kutoa mifano maana ya uhawilishaji ulalo na uhawilishaji wima.
 25. Kuvia akili ni nini?
 26. Eleza mahitaji ya mwanafunzi katika umri wa  kuanzia miaka 7 – 15.
 27. Kwa nini mwanafunzi hufundishwa stadi ya kuzungumza kabla ya kumfundisha stadi ya kuandika?
 28. Maarifa ni nini?
 29. Eleza na fafanua nadharia ya “Umwenendo”.
 30. Eleza maana ya usemi huu, “Motisho huongeza tija”.
 31. Nini umuhimu wa Elimu ya Maadili katika kujifunza?
 32. Kichocheo hasi hutolewaje?
 33. Kuna aina ngapi za motisho?
 34. Taja mambo yanayoonesha kuwa mwanafunzi amejifunza.
 35. Kuna manufaa gani kwa mwalimu kuwapa wanafunzi kazi za kufanya nyumbani?
 36. Eleza na fafanua misingi inayotumiwa wakati wa kutoa mazoezi.
 37. Tunga maswali matano (5) yanayopima ngazi ya juu ya maarifa.
 38. Taja aina tano (5) za zana unazoweza kutengeneza kutoka mazingira ya shule.
 39. Eleza manufaa ya kutumia zana wakati wa kufundisha.
 40. Taja na eleza aina mbalimbali za mbao za kufundishia.
 41. Eleza maana ya dhana. Toa mifano kusaidia ufafanuzi wako.
 42. Eleza hatua za kufuata wakati unapotaka kutatua tatizo lolote.
 43. Ubora wa njia yeyote unategemea mambo gani?
 44. Mwanafunzi anaweza kujifunza bila kuwapo kwa mwalimu. Eleza ni katika mazingira gani hali hii inaweza kutokea.
 45. Kwa mujibu wa Hurlock michezo ni nini?
 46. Jadili hitilafu tatu (3) za kuzungumza wanazopata watoto.
 47. Eleza kwa kifupi kuhusu mitihani ya insha.
 48. Eleza majukumu manne (4) ya Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC).
 49. Taja faida tano (5) za maswali yanayoulizwa na mwalimu darasani.
 50. Kujifunza huimarika kwa kuzingatia Nyanja kuu tatu (3), zitaje.

 

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

12 thoughts on “Jipime na Msawali 50 Kusherehekea Muhula Mpya 2014 | Maswali Mchanganyiko

 1. Unajitahidi sana kuwasaidia vijana walooko masomoni iwapo watatumia mda wao kufanya haya maswali unayowatungia. Hebu jaribu kuwapa na haya
  1. Eleza maana ya upimaji
  2. Fafanua maana ya upimaji katika ufundishaji na ujifunzaji
  3. Kwa kutumia mifano eleza umuhimu wa upimaji kwa mwalimu na mwanafunzi
  4. Orodhesha hatua nne muhimu katika uundaji wa mtihani na majaribio
  5. Taja hatua za kufuatawakati wa kuandaa jedwali la kutahin

  Like

 2. Rekebisha swali la pili lisomeke hivi: Fafanua manufaa ya upimaji katika ufundushaji na ujifunzaji

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.