Je, Ndoa yako ni Batili au Batilifu?

Ndoa batili

 Hii ni ndoa ambayo ni ubatili mtupu tokea mwanzo na inasababishwa na sababu zifuatazo:

 1. Kama wanandoa ni ndugu waliozuiwa kuoana.
 2. Kama mwanandoa mmoja hana uwezo wa kuoa au kuolewa kwa kuwa na ndoa nyingine inayoendelea
 3. Kama mahakama au baraza limeamua ndoa isifungwe.
 4. Kama ukubali wa mwanandoa haukuwa huru na wa hiari.
 5. Kama wanandoa wote hawapo siku ya sherehe ya ndoa.
 6. Kama kuna makubaliano ya ndoa kuwa ya muda au muda maalum.
 7. Kama mwanamke ni mjane au mtalikiwa kabla ya ndoa na ndoa yake ilifungwa kwa mujibu wa taratibu za kiislam wakati mke akiwa bado katika eda.

renoir_150

Ndoa batilifu

 Hii nii ndoa ambayo kwa namna yeyote ile ni halali lakini ina matatizo yanayoweza kumpelekea mwanadoa mmojawapo kuomba ndoa ivunjwe.

Sababu zifuatazo zinaweza kuifanya ndoa iwe batilifu:

 1. Kama mwanandoa mmoja hawezi tendo la ndoa.
 2. Kama mmojawapo ana kichaa au kifafa.
 3. Kama mwanandoa mmoja ana ugonjwa wa maambukizi.
 4. Kama mwanandoa alipata mimba kutoka kwa mtu mwingine  mbali na  mwanaume aliyemuoa.
 5. Kama tendo la ndoa halijafanyika kwa kuwa mwanandoa amekataa kufanya kwa makusudi.
 6. Kama mwanamke hajafikisha miaka 18 ma mahakama inaona kuna sababu nzuri na za kujitoshereza kuiweka ndoa pembeni.

Ikumbukwe kuwa ndoa batilifu kwa namna yeyote ile ni ndoa halali mpaka mahakama itoe tamko la kuivunja. Watoto wanaozaliwa ndani ya ndoa batilifu ni halali.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.