UONGOZI NA UENDESHAJI WA SHULE ZA MSINGI

Maana ya Shule.

   Shule ni mkusanyiko, taasisi, shirika au mahali ambapo hutoa/hutolewa mafunzo kwa watu wengi kwa wakati mmoja au nyakati mbalimbali kuhusu Elimu (msingi, sekondari, ya juu au watu wazima) kwa muda uliopangwa.

Shule ya Msingi.

            Ni chombo kinachotoa Elimu ya msingi iliyokamili (Tanzania – kwa muda wa miaka saba mfululizo) kwa kuzingatia mihtasari ya mafunzo.

Uongozi wa Shule

           Ni chombo kinachoonesha njia katika utendaji wa majukumu mbalimbali ili kuweza kuyafikia malengo husika ya shule.

Shule huweza kuwa na Malengo yafuatayo;

 • Kufundisha kwa bidii ili wanafunzi waelimike na kuweza kufaulu mitihani.
 • Kujenga, kutunza majengo na kuboresha mazingira ya shule.
 • Kusimamia vizuri mapato na matumizi ya shule.
 • Kuzalisha mali na kusimamia mgawanyo wa mapato;
 • Kudumisha uhusiano mwema na wadau mbalimbali wa elimu na shughuli za shule.

Uongozi

 • Ni upangaji na usimamizi wa ajukumu (utoaji wa dira).
 • Ni uwezo wa kuwawezesha watu wafanye mambo sahihi kwa wakati mwafaka wakiwa wenye kushawishika na wenye shauku ya kufanikiwa.
 • Ni uwezo wa kuwaelekeza na kuwahamasisha watu wengine katika jumuiya (kamati) ili kufikia lengo lililokusudiwa.

 Kiongozi wa Shule ya msingi.

 • Ndie mpangaji wa majukumu kwa walimu na wafanyakazi waliochini ya usimamizi wake.
 • Kusimamia utekelezaji wa shughuli zao zilizopangwa.
 • Kuhakikisha walimu wa madarasa na wakuu wa idara wanatimiza wajibu wao.

Uendeshaji

            Ni usimamizi mzuri wa majukumu mabalimbali yaliyowekwa.

Ikumbukwe kwamba kuongoza ni kuonyesha njia, kutanguliza na kuelekeza katika utekelezaji wa majukumu ya umma. Kuongoza ni kujenga moyo wa pamoja miongoni mwa wanaoongozwa na kuwahamasisha ili watekeleze yale yaliyokusudiwa.

Aina za Uongozi

Kuna aina mbali mbali za uongozi mashuleni kulingana na mtindo unaotumika katika kuongoza.

Kuna Mitindo mikuu minne ya Uongozi ambayo ni;

 1. Uongozi wa kiimla
 2. Uongozi wa Mahusiano mema
 3. Uongozi Uliobweteka
 4. Uongozi wa Pamoja

1. Uongozi wa kiimla,

 • Hii ni aina ya uongozi ambao Kiongozi hutoa amri na kutekelezwa na anaowaongoza bila ya wao kutoka kauli yeyote.
 • Kiongozi huyu huongoza kwa vitisho na amri kali kwa kudhani kuwa walio chini yake ni wazembe, wasiotaka kutimiza wajibu wao na kuwa na mawazo yao hayafai kuchangia katika uongozi wa shule.

Sifa za Uongozi wa Kiimla.

1.      Unatumia amri
2.      Unapenda kujilabu ( kujigamba/kuwa na imani ndogo kwa wadau)
3.      Amri zinatoka juu kuja chini
4.      Kiongozi anawagawa wafanyakazi
5.      Wakati mwingi maslahi ya wafanyakazi hayapewi uzito
6.      Hauko wazi juu ya mapato na matumizi ya shule
7.      Hauruhusu kukosolewa

Kiongozi wa Kiimla husababisha mitafaruku na migomo ya wafanyakazi.

Uongozi wa kiimla huleta ufanisi wa kinafiki na upendeleo, hujenga chuki, fitina na usengenyi baina ya wafanyakazi kwa wengi kujikomba kwa kiongozi, hapendwi kwa dhati na wafanyakazi.

2. Uongozi wa Mahusiano mema

 1. Ni aina ya uongozi unaojenga mahusiano mema baina ya kiongozi na wafanyakazi.
 2. Kiongozi anaetumia mfumo huu wa uongozi huamini kuwa ubora na ufanisi wa kazi huja pale wafanyakazi wanapoondoa tofauti zao na kufanya kazi kwa bidii na kujenga mahusiano mema.

Katika shule, kiongozi wa mfumo huu, husuluhisha matatizo baina ya wafanyakazi kwa wafanyakazi (walimu), wanafunzi na wanjumuiya wanayoizunguka shule.

3. Uongozi Uliobweteka

 1. Hii ni aina ya uongozi usiojali lolote katika utendaji wa kazi, liwe zuri au baya.
 2. Kiongozi wa aina mfumo huu hajali ufanisi wa kazi yake na wale anaowaongoza.
 3. Kiutendaji hakuna usimamizi mzuri na madhubuti wa kazi kwa wafanyakazi (walimu) na utendaji kazi huwa duni.

Viongozi wa mfumo huu huwa hawana malengo na mara nyingi husababisha shule kuzorota na wanafunzi kufeli mitihani.

4. Uongozi wa Pamoja

 1. Ni uongozi unaoshirikisha wafanyakazi wote kimawazo na kivitendo katika uongozi wa sehemu ya kazi.
 2. Mfanyakazi huwa huru na kujiona ni sehemu muhimu ya uongozi wa shule.
 3. Ugawaji wa madaraka baina ya wafanyakazi ni kitu cha kawaida.
 4. Ushirikiano katika utendaji wa kazi, uaminifu, umoja, upendo na kujiamini baina ya wafanyakazi ni matokeo mazuri ya uongozi wa pamoja.

Katika shule kiongozi anayetumia mtindo huu wa uongozi, huongoza kupitia kamati mbalimbali za shule na mara nyingi hutoa maamuzi yake kutokana na ushauri na mapendekezo mbalimbali ya kamati na viongozi walio chini yake.

Mfano wa Matokeo Bora ya Uongozi wa Pamoja;

 • Ufanisi unakuwa mzuri
 • Uhai wa shule una imarika
 • Kunakuwa na tija na ubunifu katika ufundishaji
 • Rasilimali zinatumika kwa ufanisi
 • Kunakuwa na ukweli na uwazi katika mapato na matumizi ya shule
 • Kuna hisia ya dhamana kwa vingozi

Sifa za Kiongozi wa Shule.

Mwalimu ni kioo cha wanafunzi na jamii. Mwalimu anatakiwa kuwa na tabia na mwenendo mzuri kimawazo, kimaneno na kimatendo. Mwalimu hapaswi kuwa na sifa zifuatazo;

 1. Ulevi wa kupindukia wakati wa kazi;
 2. Kuwa na tabia za kuleta aibu binafsi na kwajamii (umalaya, uzinzi, ushirikina, uvivu,);
 3. Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi;
 4. Uonevu, uchoyo na ukatili wa aina yeyote kwa wanfunzi na wafanyakazi;
 5. Upendeleo na udhalilishaji kwa wanafunzi na wafanyakazi wa jinsi tofauti;
 6. Wizi, utapeli, ulaghai, ubabaishaji na uchukuzi wa mali za umma visivyo halali;
 7. Matumizi ya lugha mbaya mbele ya wanafunzi na wafanyakazi wenzake;
 8. Uchafu wa mwili na mavazi.

Zoezi.

 1. Eleza aina kuu nne za;
  1.  Uongozi
  2. Viongozi
 2. Taja na fafanua tabia mbaya ambazo wewe kama Mwalimu hufai kuwa nazo.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

23 thoughts on “UONGOZI NA UENDESHAJI WA SHULE ZA MSINGI

 1. Hongera kwa elim hii.Binafsi nimeipenda tuungane kukemea ufisadi katika shule za msingi na sekondari

  Josephat Lusoko

  Like

 2. Majukumu ya kamati za shule yaliyoainishwa yamelenga zaidi kwa shule za umma. Endapo kuna mwongozo wowote wa uundaji wa kamati za shule binafsi ikiwa ni pamoja na majukumu ya kamati hiyo ni vizuri yakawekwa bayana ili kuondoa misuguano na wamiliki wa shule binafsi.

  Like

 3. Ahsanteni sana kwa ufafanuzi wenu. ufafanuzi wenu ni mzuri. ila nawaomba mnifafanulie juu ya namna ya kusimamia, kutunza na kugawanya rasilimali za shule.

  Like

 4. mkuu Kazi Nzuri na nimeshaanza kutumia nondo zako, ila naomba unifafanulie dhana ya ‘uongozi Wa mabadiliko ‘(transformation leadership )

  Like

 5. Naomba unisaidie faida za uongozi ulio bweteka na nisaidie namna ya kuratibu shughuli za taasisi au shirika

  Like

 6. Mkuu asante kwa elimu nzuri sana, naomba unisaidie kujua muundo wa uongozi/utawala ktk shule binafsi za msingi. naomba unitumie kwenye email yangu. (dicksonmulaki@gmail.com) Karibu kibondo-kigoma

  Like

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.