Jiandae Kwenda BTP na Maswali 50 ya Mbinu za Kufundishia Elimu ya Awali

 1. Eleza kwa kifupi maana ya Elimu ya Awali.
 2. Taja mambo muhimu manne (4) ayapatayo mtoto wa Elimu ya Awali anapojifunza kwa vitendo.
 3. Taja vigezo utakavyotumia kuchagua mbinu za kufundishia Elimu ya Awali.
 4. Unaelewa nini kuhusu muhtasari wa vitendo vya masomo?
 5. Taja misingi minne (4) ya ufundishaji na ujifunzaji katika Elimu ya Awali.
 6. Unaelewa nini kuhusu kitabu cha kiongozi cha mwalimu?
 7. Katika shule ya Msingi mwalimu anakazia sana ukimya, lakini katika darasa la Elimu ya Awali mwalimu anaambiwa asihangaishwe sana na mazungumzo ya watoto wakati wanapojifunza, kwa nini?
 8. Taja aina nne (4) za kufundisha katika darasa la Elimu ya Awali.
 9. Eleza kwa kifupi jinsi utakavyomsaidia mtoto asiyesikia vizuri darasani kwako.
 10. Mbinu za kufundishia Elimu ya Awali zina sifa za kipekee. Thibitisha.
 11. Jadili ni kwa namna gani Mwalimu anaweza kumfanya mtoto wa Elimu ya Awali kuwa tayari kujifunza.
 12. Fafanua kwa mifano maana ya usemi “Kuliongoza darasa ni kulielekeza darasa”.
 13. Katika kuliweka darasa katika hali ya kumfanya mtoto kujifunza kwa ufanisi mkubwa mwalimu sharti azingatie mambo kadhaa. Taja matano (5) tu kati ya hayo.
 14. Taja mambo manne (4) ya msingi ambayo mwalimu wa somo anapaswa kuzingatia wakati wa kuandaa somo lake.
 15. Taja faida tatu (3) azipatazo mtoto wa Elimu ya awali anapojifunza kwa vitendo.
 16. Taja vigezo vinne (4) utavyotumia kuchagua mbinu za kufundishia Elimu ya awali.
 17. Taja malengo ya ufundishaji Elimu ya Awali.
 18. Eleza maana ya upimaji kwa mtoto wa Elimu ya Awali.
 19. Taja aina kuu za upimaji wa mtoto wa Elimu ya Awali.
 20. Kwa nini ni lazima kila mtoto aanzie madarasa ya Elimu ya Awali kabla ya kuanza darasa la kwanza?
 21. Taja misingi minne (4) ya ufundishaji Elimu ya Awali.
 22. Nini tofauti kati ya mbinu za maelezo na mbinu za vitendo.
 23. Eleza jinsi mtoto wa Elimu ya Awali anavyopimwa ukilinganisha na mtoto wa shule za msingi.
 24. Taja vitendo sita (6) mtoto wa Elimu ya Awali anavyopaswa kujifunza.
 25. Nini maana ya maneno yafuatayo;
  1. Kithembe
  2. Kigugumizi
  3. Akili taahira
 26. Ufundishaji wa Elimu ya Awali ni tofauti na ule wa shule za msingi. Jadili.
 27. Mwalimu wa Elimu ya Awali anapofundisha darasa lake anashauriwa kubadili tendo mara kwa mara. Jadili.
 28. Katika shule ya msingi mwalimu anakazia ukimya wakati akifundisha. Lakini katika darasa la Awali mwalimu anaombwa asihangaishwe sana na mazungumzo ya watoto wakati wanapojifunza, kwa nini? Jadili.
 29. Eleza dhana ya Elimu ya Awali.
 30. Taja malengo matano (5) ya kufundisha na kujifunza malezi ya Elimu ya Awali kwa mwalimu Daraja ‘A’.
 31. Eleza umuhimu wa Elimu ya Awali.
 32. Nini mtazamo wa Elimu ya Awali kwa jamii ya Kitanzania?
 33. Kwa nini ongezeko la shule za awali ni kubwa mno maeneo ya mijini kuliko vijijini ambako kuna ongezeko la watu wengi?
 34. Taja wanafalsafa watano waliokuwa na mitazamo inayohusu Elimu ya Awali.
 35. Nini maana ya Mtaala wa Elimu ya Awali?
 36. Ni mambo yapi huunda Mtaala wa Elimu ya Awali?
 37. Eleza dhana ya zana za kujifunzia na kufundishia.
 38. Haki za mtoto zimegawanyika katika vipengele vitano vya msingi. Taja na kueleza haki 3 za msingi.
 39. Eleza matatizo yanayoweza kujitokeza katika utekelezaji wa mtaala wa Elimu ya Awali.
 40. Eleza mambo ya kuzingatia katika utunzaji bora wa mtoto.
 41. Nini wajibu wa Mwalimu katika kulinda haki za mtoto?
 42. Taja mambo manne (4) yanayosababisha kuwepo kwa mawasiliano katika utoaji wa Elimu ya Awali.
 43. Taja malengo matano (5) ya kufundisha na kujifunza malezi ya Elimu ya Awali kwa mwalimu Daraja ‘A’.
 44. Katika Tanzania elimu ya Awali imegawanyika katika sehemu mbili. Zitaje.
 45. Nini maana ya Haki.
 46. Katika Elimu ya Awali upimaji unakuwaje?
 47. Nini maana ya kujifunza.
 48. Taja makundi matatu (3) ya magonjwa ya watoto.
 49. Eleza kwa nini ni muhimu mwalimu kuzijua hatua za makuzi ya mtoto kiakili.
 50. Nini maana ya adhabu? Eleza faida na hasara za adhabu katika kujifunza.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Jiandae Kwenda BTP na Maswali 50 ya Mbinu za Kufundishia Elimu ya Awali

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.