Wimbo kwa Ajili ya Kuboresha Elimu- BONGO ALL STAR

Salamu toka HakiElimu!

ImageHakiElimu ni asasi ya kiraia ambayo dira yake ni kuiona Tanzania ikiwa mahali ambapo watoto wote wanapata haki yao ya kupatiwa elimu bora ya msingi, na ambapo shule zinaheshimu utu na haki za binadamu kwa wote; na ambapo elimu inalenga kujenga usawa, ubunifu, uwezo wa kuhoji na kutafakari mambo kwa undani na kwa demokrasia.

Mwaka 2013, wasanii wa muziki wa kizazi kipya kwa kushirikiana na HakiElimu tulitengeneza wimbo wa TOKOMEZA ZIRO mahususi kwa ajili ya kuelimisha wananchi ili washiriki vyema katika kuboresha elimu. Wimbo huu, ulitengenezwa na wasanii baada ya  kuona elimu yetu ikizidi kudidimia kwa kushuhudia matokeo mabovu ya kidato cha Nne na darasa la Saba kwa mwaka 2012.

Katika wimbo huo wasanii wamehamasisha wanafunzi ili wasome kwa juhudi ingawa kuna changamoto nyingi. Pia umewataka wazazi washiriki kikamilifu katika kusimamia maendeleo ya watoto wao kielimu na wananchi kwa ujumla watambue umuhimu wa elimu na kushiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya elimu. Serikali kuchukua hatua madhubutui za kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu.

Jumla ya wasanii maarufu 11 wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika kuimba nyimbo hiyo ni: Diamond, Linah Sanga, Mwasiti Almas, Peter Msechu, Lunex, Mwana FA, Kala Jeremiah, Roma Mkatoliki na Maunda Zoro.

Hivyo, tunakutumia wimbo (Bofya hapa ku Download) ili uweze kuusikiliza kwa makini, kutafakari kwa makini na  kuchukua hatua ipasavyo ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu. Pia, usambaze wimbo huu kwa wadau mbalimbali katika eneo lako. Aidha, unaweza kuhamasisha wimbo huu kupigwa katika matukio mbalimbali ya kijamii. Mwisho, unaweza kuuhifadhi wimbo huo katika simu yako na kuusambaza kwa watu mbalimbali kwa njia ya simu. Kufanya hivyo, ujumbe utakuwa umewafikia wengi.

Ukimaliza kuusambaza wimbo huo unaweza kututumia mrejesho kwa kiasi gani umefanikiwa katika kuusambaza na kwa kiasi gani wimbo huo umesikilizwa katika jamii inayokuzunguka. 

Tunatanguliza shukhurani

Kwa niaba ya Kaimu Meneja

Edwin Mashasi

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.