Maswali na Majibu – Sehemu I | Dhana ya Ualimu

DSC01466

1.       Fafanua dhana nne (4) za ualimu.

a.       Dhana ya Maelezo

Kulingana na dhana hii, ualimu ni utoaji wa maarifa na ujuzi.

b.      Dhana ya Mafanikio

Katika dhana hii kufundisha na kujifunza ni muhimu; hii ina maana kwamba kufundisha hakuwezi kukawepo bila kujifunza kuwepo.

c.       Dhana ya Makusudio

Katika dhana hii, tendo la kufundisha linahusisha kutambua umuhimu wa malengo, mawazo, na imani ya mwalimu kuwa ni vigezo muhimu katika utendaji wake wa kazi. Smith (1989) anasisitiza kuwa imani hizo ni muhimu sana katika kuleta athari katika kazi ya ualimu.

d.      Dhana ya Kisayansi

Kulingana na dhana ya kisayansi ualimu huoneshwa kwa mafanikio au athari. Ualimu hujumuisha vipengele vya uwezo wa kuleta mafanikio. Mafanikio ya ualimu ni kubadilika kwa mwanafunzi kimaadili, kiujuzi na kifikra. Ualimu usioleta au kuonesha mafanikio mema una kasoro.

2.       Taja sifa zinazomfanya Mwalimu kuwa kisima cha maarifa na ujuzi.

Sifa zinazomfanya mwalimu kuwa kisima cha maarifa na ujuzi ni;

 • Mwalimu ana utaalamu wa kumuwezesha mtoto kuanza kuhesabu, kusoma na kuandika;
 • Baadaye mwalimu humfundisha mwanafunzi maarifa ya jamii, hisabati, stadi za kazi, sayansi, afya, lugha na taaluma mbalimbali.

3.       Eleza jinsi utakavyowasaidia wanafunzi wako ambao idadi yao ni kati ya 70 – 90 wakiwa katika chumba kimoja cha darasa.

Yapo mambo mengi ambayo mwalimu anapaswa kuyafanya ikiwa ni pamoja na;

 • Kugawa wanafunzi katika vikundi ili wasome kwa zamu
 • Kutumia mbinu ya kazi mradi zaidi katika kufundisha na Kuwapa kazi nyingi za kufanya darasani za kujisomea;
 • Kufundisha kwa kuzunguka zunguka darasani kuliko kukaa mbele tu ya darasa kwani wanafunzi wengi hasa wa nyuma darasani hawawezi kusikia vizuri.

4.       Ni vipengele vipi vinavyothibitisha kushuka kwa hadhi ya walimu?

 • Kuwapa wanafunzi mimba;
 • Kulewa ovyo;
 • Kutumia lugha chafu mbele ya wanafunzi;
 • Kuvaa ovyo ovyo;
 • Kushindwa kufundisha vizuri;
 • Kushindwa kuongea kiingereza;
 • Kutojua kikamilifu maarifa ya masomo mengi na Kuuza mitihani

5.       Ni mambo gani muhimu hufanyika katika vyuo vya ualimu (Daraja A) yanayohusika na kumwandaa mwalimu tarajali wa shule za msingi?

 • Hufundishwa masomo ya Saikolojia, Falsafa ya Elimu, Msingi ya Elimu, Mitaala na Ufundishaji na Njia mbalimbali za kufundisha masomo;
 • Hujifunza kuandaa maazimio ya kazi na maandalio ya somo;
 • Hujifunza taratibu, sheria na miiko ya kazi;
 • Hufanya Mazoezi ya kufundisha.

6.       Eleza kwa kifupi changamoto nne zinazoifanya kazi ya ualimu hapa Tanzania ionekane ni kazi ngumu na isiyo na mvuto (NECTA 2011).

 • Mazingira magumu na duni ya kufanyia kazi na idadi kubwa ya wanafunzi darasani;
 • Maslahi madogo ya mishahara;
 • baadhi ya watu kujiunga na vyuo vya ualimu bila ya kuwa na sifa hivyo kuongeza mzigo kwa walimu wenzao kazini;
 • walimu wengi huacha kazi na kujiunga na kazi nyingine hivyo kuwakatisha tama walimu wengine;
 • ukosefu wa vifaa vya kufundishia na uhaba wa samani madarasani;
 • ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara kazini.

7.       Orodhesha adhabu nne zinazoweza kutolewa na Tume ya Walimu Tanzania kwa mwalimu anayekiuka maadili ya kazi ya ualimu (NECTA 2012)

 • Kufukuzwa kazi na kusimamisha uanachama wake katika utumishi,
 • Kupunguzwa kwa mshahara wake lakini sio chini ya kiwango cha kwanza katika ngazi aliyoajiriwa nayo,
 • Kuteremshwa daraja,
 • Kusimamisha au kuchelewesha nyongeza ya mshahara,
 • Onyo au karipio kali;

8.       Eleza kwa ufasaha sababu tano (5) zinazofanya ualimu uwe kazi ya kitaalamu (NECTA 2012).

 • Utaalamu hutoa huduma kwa jamii
 • Una miiko ya kazi – Utaalamu una miiko ya kazi ambayo hueleza kinaganaga uhusiano kati ya mtaalamu na mteja wake ambayo inamlinda mteja. Katika Tanzania Tume ya Utumishi wa Walimu inaeleza miiko katika kazi ya walimu na pia Chama cha Walimu kinasisitiza kimsingi udumishaji wa miiko ya walimu kazini.
 • Una utaratibu unaofahamika wa kumwendeleza mfanyakazi – kila kazi ina namna yake ya kutoa mafunzo kazini. Katika ualimu kumekuwa na mafunzo ya aina mbalimbali ya kumwendeleza mwalimu.
 • Una utaratibu mahsusi wa mawasiliano – kuanzia ngazi ya chini kabisa mwalimu anautaratibu mahsusi wa mawasiliano kuanzia kwa mwalimu mkuu hadi waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi.

9.       Eleza sifa tatu (3) za mwalimu zinazoweza kumfanya aheshimike kwa wanafunzi na wanajumuia.

 • Ana dumisha miiko na maadili ya kazi yake ya ualimu;
 • Anaipenda kazi yake na kufundisha kwa moyo;
 • Hujitolea katika kuisaidia, kuishauri na kushiriki katika shughuli za maendeleo katika jamii

10.   Eleza umuhimu wa mafunzo ya ualimu kazini kwa walimu walio kazini.

Mafunzo ya ualimu kazini husaidia;

 • Kuziba mapengo yaliyoachwa na mafunzo tarajali;
 • Kupata maarifa mapya na mabadiliko ya kielimu na kijamii yanayotokea nchini na duniani kote;
 • Kuelewa mabadailiko ya mitaala pamoja na mihtasari;
 • Kusahihisha makosa yanayotokea katika vitabu na mihtasari;
 • Kuenda na wakati katika kuelewa mbinu za kufundishia;
 • Kujifunza mbinu za utawala wa shule.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

9 thoughts on “Maswali na Majibu – Sehemu I | Dhana ya Ualimu

 1. Walimu ni watu wakubwa sana ambao wametengeneza wat maarufu hapa duniani mm nawapongeza sana na nina waomba waifanye kazi yao kwa moyo bia naomba serikali itambue kwamba pasipo walimu hatuwezi kwenda popote wala kufika popote so ningeiomba serikali iboreshe makazi ya waalimu na hata malipo yao big up sana walimu wote duniani munaojua wajibu wenu na kuwajibika mungu awatie nguvu mm na waombea kila la heri mungu awabariki sana

  Like

 2. Axante xana waandaaji, kwel taaluma ya ualimu inafaa iwapo mawazo yatakuwa yanatoka kwa wadau mbalimbali ktk swala zima la uboreshaji.

  Like

 3. Nashukuru Sana Kwa Kutusaidia Sisi Tunaofundishwa Na Bora Wakufunzi Na Sio Wakufunzi Bora. Nimepata Maarifa Mengi Sana Kupitia Nukuu Hizo. Tunakuomba Endelea Na Moyo Huo Wa Kujituma Kusaidia Walimu Tarajali. Ahsante Xana

  Liked by 1 person

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.