Maswali na Majibu – Sehemu II | Dhana ya Ualimu

 

1. Eleza matatizo matatu (3) yanayompata mwalimu asiyekuwa na vitabu vya kiada.

 • Kukosa maarifa na ujuzi wa somo;
 • Kufundisha kwa kubabaisha;
 • Kukosa kujiamini;
 • Kudharauliwa na wanafunzi

2.       Jadili athari zilizoikumba fani ya ualimu hapa nchini mara baada ya kuanzishwa kwa mipango mbalimbali ya kielimu mfano UPE (1974), Kupanuka kwa sekta ya elimu ya msingi na sekondari baada ya kuanzishwa kwa MMEM (20022006) na MMES (2004).

 • Walimu wengi waliajiriwa hivyo kusaidia kupunguza uhaba wa walimu;
 • Muda wa mafunzo ya ualimu ulipunguzwa kutoka miaka miwili hadi mwaka mmoja ili kukabiliana na uhaba wa walimu uliokuwepo;
 • Idadi kubwa ya wanafunzi waliandikishwa kuanza darasa la kwanza;
 • Idadi ya madarasa/majengo iliongezeka baada ya ruzuku kupelekwa mashuleni kuimarisha na kuongeza ujenzi wa madarasa;
 • Uhaba wa vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule baada ya ungezeko la watoto kuandikishwa;
 • Walimu wengi waliendelezwa/kijuendeleza kutoka ualimu wa Daraja C/B hadi kufikia Daraja A.

3.       Taja vitendo sita vya masomo vinavyofundishwa katika elimu ya awali.

Mabadiliko hayo yalitokana na  kuunganisha vitendo vya Haiba na vitendo vya michezo na kuwa vitendo vya Haiba na Michezo, vitendo vya Muziki kuunganishwa na vitendo vya Sanaa na kuwa vitendo vya Sanaa,  vitendo vya Afya viliunganishwa na vitendo vya Sayansi na kuwa vitendo vya Sayansi.  Hivyo basi maboresho haya yamefanya kuwa na vitendo sita (6) vya masomo kama ifuatavyo:

i) Vitendo vya Hisabati

ii) Vitendo vya Kiswahili

iii) Vitendo vya Sayansi

iv) English learning activities

v) Vitendo vya Sanaa

vi) Vitendo vya Haiba na Michezo

4. Kwa mujibu wa sera ya elimu na mafunzo ya 1995, fafanua sifa tatu (3) za kujiunga na mafunzo ya ualimu nchini.

 • Awe amemaliza kidato cha nne na kufaulu si chini ya divisheni ya tatu;
 • Awe ameomba mwenyewe kujiunga na ualimu;
 • Awe ni kijana mwenye mwenendo na tabia nzuri;
 • Awe mtu anayeweza kujituma kwa kuwa anatarajiwa kukabidhiwa vijana na kuwasimamia.

5. Eleza kwa kifupi aina mbili (2) za mafunzo ya Ualimu nchini.

Mafunzo ya ualimu nchini yamegawanyika katika makundi makuu mawili;

 • Mafunzo ya mwalimu tarajali – yaani kabla ya mtu kuanza kazi.
 • Mafunzo ya mwalimu kazini – yaani  wakati mtu anaendelea kufanya kazi.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Maswali na Majibu – Sehemu II | Dhana ya Ualimu

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.