Swali na Jibu | Njia za Unasihi (NECTA 2004)

Eleza njia tatu (3) zinazoweza kutumiwa katika kutoa ushauri kwa mtu au watu. (NECTA 2004)

1)      Mshauriwa kama kiini cha nasaha (Client centered counseling technique).

Mteja husaidiwa kuelewa tatizo lake, kulikubali, kulipokea, kutafuta mbinu za utatuzi zinazowezekana na kutoa mchango wa mawazo ya mikakati ya kutekeleza utatuzi uliofikiwa kwa pamoja.

Katika njia hii, mteja huwa mzungumzaji mkuu wakati shughuli kuu ya mnasihi ni kusikiliza, kumsaidia na kuweza kupata mbinu bora ya ufumbuzi wa kutatua tatito lake.

2)      Mshauri kama kiini cha nasaha (Counselor centered counseling technique).

Katika njia hii, mnasihi hutumia nafasi kubwa wakati wa shughuli ya kunasihi. Mnasihi humdodosa mteja wake ili kufanya uchambuzi wa chanzo cha tatizo la mteja wake, ili aweze kumpa mteja maoni ya njia na hatua nzuri atakazotumia kutatua tatizo lake.

3)      Njia ya mseto (Eclectic counseling technique).

Njia hii huunganisha njia mbili za awali kwa vile kila njia ina ubora wake kutegemea aina ya mteja, tatizo, mazingira na ustadi wa mnasihi.

Author: Sir Gunda

A Friend of Education

One thought on “Swali na Jibu | Njia za Unasihi (NECTA 2004)

Usikae kimia sema kitu juu ya nukuu hizi

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.