Eleza njia tatu (3) zinazoweza kutumiwa katika kutoa ushauri kwa mtu au watu. (NECTA 2004)
1) Mshauriwa kama kiini cha nasaha (Client centered counseling technique).
Mteja husaidiwa kuelewa tatizo lake, kulikubali, kulipokea, kutafuta mbinu za utatuzi zinazowezekana na kutoa mchango wa mawazo ya mikakati ya kutekeleza utatuzi uliofikiwa kwa pamoja.
Katika njia hii, mteja huwa mzungumzaji mkuu wakati shughuli kuu ya mnasihi ni kusikiliza, kumsaidia na kuweza kupata mbinu bora ya ufumbuzi wa kutatua tatito lake.
2) Mshauri kama kiini cha nasaha (Counselor centered counseling technique).
Katika njia hii, mnasihi hutumia nafasi kubwa wakati wa shughuli ya kunasihi. Mnasihi humdodosa mteja wake ili kufanya uchambuzi wa chanzo cha tatizo la mteja wake, ili aweze kumpa mteja maoni ya njia na hatua nzuri atakazotumia kutatua tatizo lake.
3) Njia ya mseto (Eclectic counseling technique).
Njia hii huunganisha njia mbili za awali kwa vile kila njia ina ubora wake kutegemea aina ya mteja, tatizo, mazingira na ustadi wa mnasihi.
Its nice
LikeLike
Je umuhimu wa njia hizi ni upi??
LikeLike