Eleza umuhimu wa kutoa ushauri nasaha kwa wanafunzi wa shule ya msingi, hususani wale wenye matatizo ya kielimu na kifamilia. (NECTA 2004)
1) Husaidia wanafunzi kujielewa kulingana na hali walizonazo ili kuwasaidia.
2) Huongeza utambuzi wa mwanafunzi wa nafsi yake kuhusiana na wengine.
3) Husisitiza mahusiano kati ya matakwa ya kielimu na maendeleo ya binafsi.
4) Hukuza utambuzi bora wa mwanafunzi kwa familia yake.
5) Hutoa/huwezesha hisia za usalama na namna ya kuishi kwa amani katika familia.
6) Huongeza jitihada za mwalimu katika kusaidia matatizo ya watoto.